Watumiaji wengi wa TikTok Marekani wamemtusi Mark Zuckerberg kwa kumuita mjusi wakidai yeye ndiye mfitini mkubwa wa TikTok kufungiwa

Watumiaji wengi wa TikTok Marekani wamemtusi Mark Zuckerberg kwa kumuita mjusi wakidai yeye ndiye mfitini mkubwa wa TikTok kufungiwa

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Idadi kubwa ya watumiaji wa TikTok Marekani wamemtusi Mark Zuckerberg kwa kumuita mjusi wakidai yeye ndiye mfitini mkubwa wa TikTok kufungiwa ili kampuni yake ya META iongeze watumiaji

Watumiaji hao wamedai hawako tayari kutumia bidhaa za META na wengi wamefuta Application zake katika simu zao wakidai ni fedhuli mkubwa na vilevile products zake zimepitwa na wakati hasa Facebook wanayoishutumu kama mtandao wa kizee usiofaa kutumiwa na vijana wa kisasa

Wameenda mbali na kudai watatumia mitandao mingine kama Rednote, Telegram na Signal mbadala wa mitandao yake
1000059627.jpg
1000059629.jpg
1000059630.jpg
1000059631.jpg
 
Wanaipenda TikTok kuliko products zake wanadai yeye ndiye aliyefitini TikTok ifungwe ili abaki yeye
Duh hatari sana kwakweli inamana imefungiwa kabisa, ila katika bidhaa za meta iliobora kidogo ni IG tu. Mkuu hivi kuna app nyingine ambaye inafanana na whatsapp?
 
Story ya mjusi ni ndefu sana.

Kuna conspiracy theory kwamba kuna mijusi ambayo imejibadilisha kuonekana kuwa watu, na mijusi hiyo ndiyo inai control dunia.

Kwa habari zaidi anzia hapa.

Dah kuna mambo yana ukakasi sana kweli nimerudi nimetizama baadhi ya picha za huyu mtaalam wa meta aisee yale macho yamekaa ki namna flani hivi ambayo sio kawaida.
 
Dah kuna mambo yana ukakasi sana kweli nimerudi nimetizama baadhi ya picha za huyu mtaalam wa meta aisee yale macho yamekaa ki namna flani hivi ambayo sio kawaida.
Hahaa. Washakuchota naona.

Hizo ni stories za Conspiracy Theories tu.

Kuna wakati wa urais wa George W. Bush huku watu walikuwa wanaamini kabisa "George W. Bush is a lizard".
 
Hahaa. Washakuchota naona.

Hizo ni stories za Conspiracy Theories tu.

Kuna wakati wa urais wa George W. Bush huku watu walikuwa wanaamini kabisa "George W. Bush is a lizard".
Hawa watu jamii ya lizard mbona wanahusishwa na illuminati,, ambapo George w Bush anahusishwa na illuminati pengine ni kweli na sio masimulizi ya kupita huyu George Bush wanasema ni mwanachama wa skull ☠️ and bones nadhani pia kwa huko U. S. A hata masonic temple zipo available so unaweza kuwa unajua vizur kama ni conspiracy theories au la.
 
Mkuu,

Na wewe unaamini George W. Bush na Mark Zuckerberg ni lizards? 😂😂😂
 
Yaani comments chache za hao wahuni zinakufanya wewe uhitimishe kuwa hayo ndio maoni ya wamarekani.....????
 
Back
Top Bottom