Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Cha kujiuliza mkuu, kutoza hiyo laki unusu ilikuwa ni kipendaroho chao hao staff au ni sera ya Wizara ya afya kuchangia matibabu?Kusimamishwa haitoshi, hadi sasa walitakiwa wawe wamesha kamatwa na kesho wafikishwe mahakamani.
nakubaliana na wewe, ninachopinga eti gharama za wajawazito, watoto, wazee ni bure. Stupid waongoSio Bure but alitakiwa apatiwe Huduma then aandikiwe deni siku ya kutoka atoe ndo atolewe. Kuna jirani yangu mmoja mkewe kajifungua mpaka sasa kazuiliwa hosp kisa hela Hana. Mmewe ni jobless ni kibaka. Hata vifaa vya kujifungulia majirani ndo wameungaunga. Kazuiliwa but kikubwa keshajifungua
Familia ile ni masikini sana, hawawezi kuacha kutafuta cha kula waende mahakamani.Je, familia ya marehemu wanaweza kufungua docket ya kumshitaki waziri wa Afya kwa tukio hili ambalo serikali imeshakiri kuwa kulikua na uzembe?,yaani nikiifikiria nchi yangu hii na watanzania hawa,nakata tamaa kabisa, royal families hawapati haya kwa sababu wao ni india, UK, Canada au Netcare Millpark,ndiko wanakotibiwa
Umesema ukweli ambao wanasiasa wanafki hawahutaki, tangu lini wakatoa hizo huduma bure? Hapo wanataka waonekane wanajali sana lakini bure kabisaStop that nonsense, huduma siyo bure, hawa siyo wapuuzi kumtoza 150,000. Kuweni wakweli
Mkuu....Cha kujiuliza mkuu, kutoza hiyo laki unusu ilikuwa ni kipendaroho chao hao staff au ni sera ya Wizara ya afya kuchangia matibabu?
Wasifanywe mbuzi wa kafara wakati sera za huduma ya afya ya umma ni mbovu.
Huu msala alitakiwa kuangushiwa Waziri wa afya mwenyewe.
Hizo 150,000 bila shaka ni gharama za mchakato wa mama kujifungua.Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kifo cha mjamzito na kichanga chake, kilichotokea Wilaya ya Handeni Tanga tarehe 11/11/2023 katika kituo cha Afya Kabuku kwa kinachoelezwa kuwa ni uzembe wa watumishi wa kituo hicho.
Pia soma > Tanga: Mjamzito afariki kwa kukosa Tsh. 150,000
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Waziri Kindamba ametuma Timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa inayojumuisha Madaktari bingwa wawili - Daktari Bingwa wa Wanawake na Uzazi na Daktari Bingwa wa Huduma za Usingizi - ili kufanya uchunguzi wa tukio hili.
Pili, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni tayari amewasimamisha kazi watumishi watatu (3) walioshiriki kumpatia huduma mama huyo tangu alipopokelewa kituoni hadi umauti ulipomkuta ili kupisha uchunguzi wa tukio hili baya na lisilopaswa kuvumiliwa!
Tatu, Tuhuma hizi pia tayari zimeshapokelewa na Mabaraza ya kitaaluma (Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC)) na vyombo vingine vya dola kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hivyo, ninaelekeza Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) ndani ya Siku 7 kuanzia leo kuniletea Taarifa ya Uchunguzi wa tukio hili na mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Nne, nataka niwahakikishie umma wa watanzania kuwa baada ya kupokea taarifa ya Uchunguzi, kila mtumishi aliyehusika atachukuliwa hatua kali za kitaaluma, kiutumishi na kijinai ikiwemo kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kijinai pale itakapothibitika hivyo.
Nichukue fursa hii kuwakumbusha watumishi wa Afya kote nchini wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Nawapa pole familia iliyoguswa na msiba huu na niahidi kuwa serikali itaendelea kusimamia ubora wa huduma za afya ili kufikia matarajio ya wananchi.
Unaongea tu inaonekana hujawahi fika hospital haswa upande wa wazazi wana walinzi na huwezi toka na mtoto bila mlinzi kukagua kalatasi za ruksa.Kibaka muda wa kupiga pumbu anaupata wapi??na hivi Hospital wakikushikilia huwezi kutoroka??naomba siku waje wamshikilie mgonjwa wangu au mimi mwenyewe nitakachowanya hawataamini!!!kwa mfano kwa hiyo isu ningekuwa mimi ndio Mume wa huyo Mama kichanga ningewaita hao Manesi waliomshikilia Mke wangu na ningewaambia mimi Pesa ya kuwapa sina,mimi na Mke wangu tunaondoka tunawachia mtoto mumlee wenyewe,simple tu
Ni shida kibaka ni kjana mdogo Hana wazazi ndugu wote wamemtenga kwa sababu hata wao alishawapiga matukio binti nae ni mdogo ndo wote uzazi wa kwanza huo. Binti kapelekwa hospital na majirani akiwa Hana hata vifaa vya kujifungulia Wala Senti Tano. Wamama ndo wamefanya kumsaidia vitenge vilivyotumika. Yaani it's so sad kwa kweli na hata akitoka hosp Huduma za mtoto home sjui atazipataje maana hata kula kwako ni kwa shida mnoKibaka muda wa kupiga pumbu anaupata wapi??na hivi Hospital wakikushikilia huwezi kutoroka??naomba siku waje wamshikilie mgonjwa wangu au mimi mwenyewe nitakachowanya hawataamini!!!kwa mfano kwa hiyo isu ningekuwa mimi ndio Mume wa huyo Mama kichanga ningewaita hao Manesi waliomshikilia Mke wangu na ningewaambia mimi Pesa ya kuwapa sina,mimi na Mke wangu tunaondoka tunawachia mtoto mumlee wenyewe,simple tu