Watumishi 3 wasimamishwa kazi kwa kusababisha Kifo cha Mjamzito kisa hajatoa Tsh. 150,000

Watumishi 3 wasimamishwa kazi kwa kusababisha Kifo cha Mjamzito kisa hajatoa Tsh. 150,000

Kusimamishwa haitoshi, hadi sasa walitakiwa wawe wamesha kamatwa na kesho wafikishwe mahakamani.
Cha kujiuliza mkuu, kutoza hiyo laki unusu ilikuwa ni kipendaroho chao hao staff au ni sera ya Wizara ya afya kuchangia matibabu?

Wasifanywe mbuzi wa kafara wakati sera za huduma ya afya ya umma ni mbovu.

Huu msala alitakiwa kuangushiwa Waziri wa afya mwenyewe.
 
Hao wanafanywa tu mbuzi wa kafara , tatizo ni utaratibu mbovu katika mahospitali yetu , fedha kwanza huduma baadae haijalishi umezidiwa kiasi gani , hizi kesi hua zinatokea sana wagonjwa kufia kaunta , sio wajawazito pekee. Uongozi mzima uwajibishwe hao walikua wanatekeleza jinsi walivyo pangiwa ma viongozi wao
 
Sio Bure but alitakiwa apatiwe Huduma then aandikiwe deni siku ya kutoka atoe ndo atolewe. Kuna jirani yangu mmoja mkewe kajifungua mpaka sasa kazuiliwa hosp kisa hela Hana. Mmewe ni jobless ni kibaka. Hata vifaa vya kujifungulia majirani ndo wameungaunga. Kazuiliwa but kikubwa keshajifungua
nakubaliana na wewe, ninachopinga eti gharama za wajawazito, watoto, wazee ni bure. Stupid waongo
 
Ummy acha uhuni Unajua kabisa kuwa bure hakuna huko! Acheni anasa kwa kutumia pesa za jasho letu kwa vitu vya anasa kama, malipo kwa wenza wa wastaafu, magari ya anasa, ufisadi na wizi wa pesa zetu nyingi tu, akiongoza waziri wa pesa Nchemba! Toeni kipau mbele kwa vitu vya msingi, ikiwemo mama na mtoto. Wapi Toto Afya? Unamaana nchi haina uwezo wa kugharamia Toto afya?

Shame on this government and its leaders! Big SHAME!
 
Tatizo halipo kwa watoa huduma Bali ni mfumo mbaya unaoendeshwa na serikali kwa kuweka gharama kubwa za afya kwaan awali mama mjamzito alikuwa ana tibiwa bure,saiz ukiangalia bima ya nhif kwa watoto ilikuwa 54,000 kwa mwaka lakini saiz package zake znaenda laki 3 na point, kwahiyo serikali kwenye nshu ya afya kwa watanzania masikini haijatilia maanani hii imetiliwa maanani kwa watumishi wa umma na matajiri ijapo baadhi ya dawa bima haiidumii Ila kwa masikini na wimbi la vijana ambao Hawa ajira ijapo wamesoma nshu ya gharama za matibabu imekuwa ni changamoto
 
Hivi hawa mawaziri wanavyosema huduma ni Bure hawana ndugu wanaoenda hizi hospital na kutozwa hela au cycle yote ya Mawaziri ni vibopa wa Premium insurance hawajui shida ? Nakumbuka nilichajiwa hela nyingi seketure Mwanza kwaajili ya dawa na sindano za mtoto wa Wiki moja wakati wao wanasema huduma ni bure, nilliandika hadi barua kwa mganga mkuu kupinga ile Invoice/Control number mwisho wa siku waliitoa kama gharama za matibabu na wakaiita gharama za Kitanda kwa kipindi ambacho walilazwa, baada ya hapo dogo nilimkatia Bima ila nasikitika hata Bima yenyewe ya Toto Afya Card wameiingizia siasa! ETI SERIKALI YA MAMA ????
 
Wakati wote tunaona makosa ya watoa huduma tuu, vipi sera zinazoleta mkanganyiko wa utoaji huduma za bure? Miongozo yetu ina tatizo, ila sina hakika kama kutomfanyia upasuaji kwa sababu ya kupewa pesa ndio iwe main cause ya kusababisha KIFO
 
Je, familia ya marehemu wanaweza kufungua docket ya kumshitaki waziri wa Afya kwa tukio hili ambalo serikali imeshakiri kuwa kulikua na uzembe?,yaani nikiifikiria nchi yangu hii na watanzania hawa,nakata tamaa kabisa, royal families hawapati haya kwa sababu wao ni india, UK, Canada au Netcare Millpark,ndiko wanakotibiwa
Familia ile ni masikini sana, hawawezi kuacha kutafuta cha kula waende mahakamani.
Hapa wa kushitakiwa ni serikali ya CCM kwa kusema uongo kwamba huduma za afya kwa mama wajawazito na watoto ni bure, hii case wanaweza kufungua wanasheria wa haki za binadamu.
 
CCM ni waongoooo,huku utasikia elimu bure,Afya bure 🚮🚮🚮
 
Vitendo kama hivi vya wauguzi kuomba pesa kwa wagonjwa zipo hospitali nyingi hapa nchini,na usipo tekeleza hongo hiyo basi utacheleweshewa huduma...kitendo hiki upelekea athari nyingi kwenye jamii.hivyo tunaiomba serikali kufatilia suala hili kwa umakini hususani huko vijijini
 
Stop that nonsense, huduma siyo bure, hawa siyo wapuuzi kumtoza 150,000. Kuweni wakweli
Umesema ukweli ambao wanasiasa wanafki hawahutaki, tangu lini wakatoa hizo huduma bure? Hapo wanataka waonekane wanajali sana lakini bure kabisa
 
Wamewapumzisha kwa muda baadae wanarudishwa kwa kubadilishiwa vituo vya kazi.
 
Kila mmoja hataki kubeba mzigo wa lawama, TZ ukiugua kama huna kitu jihesabie wewe ni maiti, vijijini huko huwezi amini kupata elfu kumi siyo mchezo, kwanza watu wana chakula tu ila unakuta pesa hawana hata uwape mwezi hiyo pesa isingepatikana...nchi ya kurushiana lawama Kwa wasiostahiki si nchi ya kujivunia kabisa.
 
Cha kujiuliza mkuu, kutoza hiyo laki unusu ilikuwa ni kipendaroho chao hao staff au ni sera ya Wizara ya afya kuchangia matibabu?

Wasifanywe mbuzi wa kafara wakati sera za huduma ya afya ya umma ni mbovu.

Huu msala alitakiwa kuangushiwa Waziri wa afya mwenyewe.
Mkuu....
Sera ya afya inampa mama mjamzito free tiba kuanzia anapo jipata mjamzito hadi anapo jifungua.
Pia inampa free tiba mtoto anae zaliwa hadi anapo fikisha umri wa mwaka nne.
 
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kifo cha mjamzito na kichanga chake, kilichotokea Wilaya ya Handeni Tanga tarehe 11/11/2023 katika kituo cha Afya Kabuku kwa kinachoelezwa kuwa ni uzembe wa watumishi wa kituo hicho.

Pia soma > Tanga: Mjamzito afariki kwa kukosa Tsh. 150,000

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Waziri Kindamba ametuma Timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa inayojumuisha Madaktari bingwa wawili - Daktari Bingwa wa Wanawake na Uzazi na Daktari Bingwa wa Huduma za Usingizi - ili kufanya uchunguzi wa tukio hili.

Pili, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni tayari amewasimamisha kazi watumishi watatu (3) walioshiriki kumpatia huduma mama huyo tangu alipopokelewa kituoni hadi umauti ulipomkuta ili kupisha uchunguzi wa tukio hili baya na lisilopaswa kuvumiliwa!

Tatu, Tuhuma hizi pia tayari zimeshapokelewa na Mabaraza ya kitaaluma (Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC)) na vyombo vingine vya dola kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hivyo, ninaelekeza Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) ndani ya Siku 7 kuanzia leo kuniletea Taarifa ya Uchunguzi wa tukio hili na mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Nne, nataka niwahakikishie umma wa watanzania kuwa baada ya kupokea taarifa ya Uchunguzi, kila mtumishi aliyehusika atachukuliwa hatua kali za kitaaluma, kiutumishi na kijinai ikiwemo kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kijinai pale itakapothibitika hivyo.

Nichukue fursa hii kuwakumbusha watumishi wa Afya kote nchini wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Nawapa pole familia iliyoguswa na msiba huu na niahidi kuwa serikali itaendelea kusimamia ubora wa huduma za afya ili kufikia matarajio ya wananchi.
Hizo 150,000 bila shaka ni gharama za mchakato wa mama kujifungua.

Kwa mujibu wa taratibu za wizara ya afya ni nani anawajibika kulipia?

Je, malipo yapo kwenye mwongozo ama wahudumu( wagaga na manesi) wamejitungia?

Kwa kumbukumbu zangu za karibuni , mimi na watu wangu wa karibu tumewahi kulipishwa kiasi kama hicho cha fedha kwa wajawazito.

Nyakati kama hizi wanasiasa hubadilika kama vinyonga na kuwaumiza watumishi kwa maslahi yao ya matumbo
 
Kibaka muda wa kupiga pumbu anaupata wapi??na hivi Hospital wakikushikilia huwezi kutoroka??naomba siku waje wamshikilie mgonjwa wangu au mimi mwenyewe nitakachowanya hawataamini!!!kwa mfano kwa hiyo isu ningekuwa mimi ndio Mume wa huyo Mama kichanga ningewaita hao Manesi waliomshikilia Mke wangu na ningewaambia mimi Pesa ya kuwapa sina,mimi na Mke wangu tunaondoka tunawachia mtoto mumlee wenyewe,simple tu
Unaongea tu inaonekana hujawahi fika hospital haswa upande wa wazazi wana walinzi na huwezi toka na mtoto bila mlinzi kukagua kalatasi za ruksa.
 
Ni shi
Kibaka muda wa kupiga pumbu anaupata wapi??na hivi Hospital wakikushikilia huwezi kutoroka??naomba siku waje wamshikilie mgonjwa wangu au mimi mwenyewe nitakachowanya hawataamini!!!kwa mfano kwa hiyo isu ningekuwa mimi ndio Mume wa huyo Mama kichanga ningewaita hao Manesi waliomshikilia Mke wangu na ningewaambia mimi Pesa ya kuwapa sina,mimi na Mke wangu tunaondoka tunawachia mtoto mumlee wenyewe,simple tu
Ni shida kibaka ni kjana mdogo Hana wazazi ndugu wote wamemtenga kwa sababu hata wao alishawapiga matukio binti nae ni mdogo ndo wote uzazi wa kwanza huo. Binti kapelekwa hospital na majirani akiwa Hana hata vifaa vya kujifungulia Wala Senti Tano. Wamama ndo wamefanya kumsaidia vitenge vilivyotumika. Yaani it's so sad kwa kweli na hata akitoka hosp Huduma za mtoto home sjui atazipataje maana hata kula kwako ni kwa shida mno
 
So sad,Yani watumishi wengi wa umma wako hivo.Wao kutimiza majukumu yao kwa wateja wao Mara nyingi Ni mtihani,wanatoa Kama msaada badala ya haki kwa yule anayemuhudumia.Kwangu kusimamishwa Mara nyingi wanasimamishwa Sana tu na hakuna mabadiliko ktk utendaji wao kiueledi na kufata kanuni na taratibu za kazi,tunaona yakijirudia kila mwaka.
Kwangu 2019 mdogo wangu alilazwa na kufanyiwa operation kwenye hospitali ya mkoa Fulani kubwa kabisa.Badae akapata changamoto ya kuvimba upande wa uso alipomwambai nesi wa zamu alijibiwa vibaya na kuambiwa Hana muda huo wa kumshugulikia.Bahati nzuri mdogo wangu alinipigia simu na kwenda mda huo huo nilipofila wodi ya Akina mama wajawazito tukaonana na huyo nesi na nikamtaka atamke Yale aliyomtolea mdogo wangu akaleta ujuaji wa kuleta kelele na wagonjwa wakanambia Yani Bora umekuja wanatutukana Sana tu,nilikuambia moja akipoteza Manisha na wewe upotee.Badae nilienda kwa mganga mfawidhi nikamwambia aitwe na aonywe vinginevyo naenda mbele zaidi badae wakamhudumi vizuri tu na akapona.

Sasa ebu angalia hii Hali Kama huna ubavu na ujasili wa kufanya hivyo si wanakuacha utabike bila msaada,inauma Sana Tena Sana kusikia mama njamzito anapoteza Manisha kwa uzembe wa watu Tena wanaolipwa kwa ajili hiyo.

Mimi hapa nalia na usimamizi wa hizi hospitali zetu yaani uongozi mzima wa hizi hospitali Yani usimamizi si nzuri na pia walio chini yao hawasimamiwi vizuri na Na kuwajibishwa do maana hawaogopi kufanya makosa Kama haya Hadi kusababisha maafa.So sad,poleni Sana wafiwa wote.
 
Back
Top Bottom