Watumishi 4,380 walioondolewa kimakosa warejeshwa kazini

Watumishi 4,380 walioondolewa kimakosa warejeshwa kazini

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amesema Watumishi 4,380 walioondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa wakati wa uhakiki wa Vyeti vya Elimu na Watumishi hewa wamerejeshwa kazini.

Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Mikumi, Dennis Lazaro Londo aliyeuliza idadi ya Watumishi waliorejeshwa kazini baada ya kuondolewa kimakosa wakati wa uhakiki wa Vyeti feki na Watumishi hewa.

Amesema, "Idadi hii inajumuisha Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa wapatao 3,114. Pia Serikali ilitoa msamaha wa kuwarejesha kazini walioondolewa kwa kukosa sifa za Kidato cha Nne ambao hawakudanganya au kughushi Vyeti".

1630396801538.png
 
Wengi watakaorudi ni wale waliopata ajira kwa cheti cha la saba
 
Bado waliovunjiwa nyumba zao kwa kiburi hapa Kimara.

Mh. Rais Hawa nao wanastahiki kulipwa fidia. Mbunge wa ubungo sijui mlimuokota wapi.
 
Bado waliovunjiwa nyumba zao kwa kiburi hapa Kimara.
Mh. Rais Hawa nao wanastahiki kulipwa fidia. Mbunge wa ubungo sijui mlimuokota wapi.
Na wakilipwa hao,Bado mtamlaumu Rais, maana hamna shukurani kabisa enyi watu
 
kuna wakati nawapenda BOKO HARAMU....... wanateka wanawake wengiiii.......then wanajaza mimba na kuwaachia uraiani.....wengi wanarudi na watoto zaidi ya watatu........hawa watoto ni lazima wakawasalimie wazazi wao......BOKO inaongezeka kwa akili njema.......kuna siku utasikia waziri fulani ni mtoto wa boko boko....ndio.......na ni mnaigeria mwenzao.....hao watumishi wamesota sana mahakamani....wengine walianzaga kabla ya mwendazake.....mirathi NIL....leo tunadanganywa tunarudishwa......4000....ni ikundi kizuri sana cha vita....mnisamehe.....ila inaudhi sana...
 
Na wakilipwa hao,Bado mtamlaumu Rais, maana hamna shukurani kabisa enyi watu
You reason like a goat.
Tulikua na kosa gani zaidi ya Mnyika kumshinda mgombea wa CCM.?
Msivyojua Ni kwamba katika waliovunjiwa wako ambao hawakupiga kura vile vile wapo wachache waliompigia kura mgombea wa CCM.
Next time read the contents carefully, understand and then comment if you must.
 
kuna wakati nawapenda BOKO HARAMU....... wanateka wanawake wengiiii.......then wanajaza mimba na kuwaachia uraiani.....wengi wanarudi na watoto zaidi ya watatu........hawa watoto ni lazima wakawasalimie wazazi wao......BOKO inaongezeka kwa akili njema.......kuna siku utasikia waziri fulani ni mtoto wa boko boko....ndio.......na ni mnaigeria mwenzao.....hao watumishi wamesota sana mahakamani....wengine walianzaga kabla ya mwendazake.....mirathi NIL....leo tunadanganywa tunarudishwa......4000....ni ikundi kizuri sana cha vita....mnisamehe.....ila inaudhi sana...
Umejitahidi kucomment ila mfano wako haujaleweka kabisa kuna sentensi za kulinganisha ujumbe wako umesahau kuziandika.
 
Ipo siku tu uchungu wa watanzania utafika kikomo na wanasihasa watakiona cha moto...

hawa jamaa wanapiga hela sio kawaida oooh my Africa
 
Mpaka hewa wamerudishwa kazini? Mbona wapo mitaani na shughuli zao walizoziashisha kujikimu kimaisha? Ina maana serikali imeandaa fungu la fedha za kujikimu hadi majina yao yarudi kwenye payrall? Vipi kuhusu fidia italipwa?
 
Duh... Kitaalamu hii sijui tunaiitaje... RIP Mwl. Kashasha.
 
Kuna mmoja nilimpa hizi taarifa akaenda kwa mkurugenzi kuulizia ila hakumkuta akaenda ofisi ya afisa utumishi akaambiwa taarifa hizo hawana waati kuna waraka ulitoka tangu mwezi wa 5 ukiwajulisha wakurugenzi na wakuu wa idara suala hili la kuwarudisha kazini
 
Back
Top Bottom