KERO Watumishi ajira mpya Halmashauri ya Chato, tunaulizia fedha za kujikimu. Tumechoka kila mara kuandika barua

KERO Watumishi ajira mpya Halmashauri ya Chato, tunaulizia fedha za kujikimu. Tumechoka kila mara kuandika barua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Idara ya Maendeleo ya Jamii, bado hatujalipwa kabisa Fedha za kujikimu hadi sasa katika kipindi cha miaka mingi sana. Tangu tumeajiriwa mwaka 2023, mwaka 2024, mwaka 2025, na mwaka huu 2026.

KERO, yetu ni hiyo yaani kila muda tunaulizia, wanasema andikeni Barua.. Ukweli ni kwamba Barua tumeshaandika nyingi sana na hatujawahi kulipwa kabisa hizo Fedha tunapitia changamoto.

Jambo lingine yaani wakiona kuna Ukaguzi au kuna Kiongozi mkubwa anakuja eneo karibu na Halmashauri ya Wilaya ya CHATO wanatoa taarifa watumishi wote wanaodai Fedha za Kujikimu andikeni Barua tunaandika lakini, hakuna Malipo yoyote.
 
Back
Top Bottom