KERO Watumishi Halmashauri ya mji Njombe tunacheleweshewa kushughulikiwa madai yetu na Maafisa Utumishi kwa makusudi

KERO Watumishi Halmashauri ya mji Njombe tunacheleweshewa kushughulikiwa madai yetu na Maafisa Utumishi kwa makusudi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya Watumishi tunaomba kufanyiwa Re-Cotegorization tangu mwezi Machi mpaka sasa hakuna mabadiliko yoyote, na tukijaribu kufuatilia unakuta barua zimenasa masijala tu. Hali hii inashusha morali sababu watumishi Halmashauri nyinginezo ambao wana madai sawa na yetu ni tayari yameshashughulikiwa

Pia, Baadhi ya watumishi wa Ajira mpya wa 2025 Elimu hawakulipwa mishahara yao ya kwanza walipoingia kazini, na wanapojaribu kufuatilia Maafisa utumishi hawatoi Ushirikiano mzuri.

Natoa wito wao kujitahidi kuweka mambo sawa ya watumishi na sio kuleta uzembe maofisini.
 
Back
Top Bottom