A
Anonymous
Guest
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (Mufindi DC) tulioajiriwa tangu mwanzoni mwa mwaka 2025 hadi sasa hatujapokea barua za kuthibitishwa kazini, licha ya kuwa tumetimiza vigezo vinavyohitajika.
Kila tunapofuatilia suala hilo kwa uongozi, hatupati majibu ya kuridhisha kuhusu sababu za kuchelewa kwa barua hizo. Hali hiyo inatunyima fursa mbalimbali zinazohitaji uthibitisho rasmi wa ajira, licha ya kuwa tunakidhi vigezo vya kuthibitishwa kazini.
Tunaomba uongozi wa Halmashauri pamoja na mamlaka husika kufuatilia suala hilo na kutoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha ucheleweshaji huo, ili hatua stahiki zichukuliwe na barua zetu zitolewe kwa wakati.