KERO Watumishi Hospitali ya Kitete (Tabora) hatulipwi stahiki zetu kwa wakati

KERO Watumishi Hospitali ya Kitete (Tabora) hatulipwi stahiki zetu kwa wakati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni kweli hospital inakusanya mapato kwa wingi lakini sisi watumishi tunadai stahiki zetu kwa muda mrefu tu hatulipwi extra duty na call allowance tangu 2024, 2025 na 2026.

Ikitokea zimelipwa ni malipo ya mwenzi mmoja na mingine unayobakia hatulipwi, tukidai wanasema madeni yetu yapo wizarani.

Tuna hali mbali Viongozi tatueni changamoto hii na sio Maneno ya siasa tu, hali hii imefanya utendaji wa watumishi kua mbaya miaka na miaka
 
Ndugu viongozi na wadau husika, tunaomba tupaziwe sauti kuhusu changamoto kubwa tunazopitia sisi watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete (Kitete RRH) katika suala la malipo ya stahiki zetu za kazi.

Kumekuwa na ucheleweshaji mkubwa wa malipo ya Extra Duty, Call Allowance, fedha za likizo pamoja na posho za usafirishaji wa wagonjwa wa rufaa kutoka kituo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano, malipo ya Extra Duty na Call Allowance tangu mwezi Januari mwaka jana hayakulipwa kwa wakati, na baada ya malalamiko ya muda mrefu walilipa mwezi Julai 2025 pekee huku miezi ya Februari, Machi, Aprili, Mei na Juni ikiachwa bila malipo hadi sasa.

Kinachowaumiza zaidi wafanyakazi ni namna malipo ya Extra Duty yanavyofanyika. Mfano, mtumishi anafanya Extra Duty ya siku 7, anajaza fomu na kusainishwa rasmi kuwa anastahili kulipwa siku zote 7 alizofanya. Lakini cha kushangaza, wakati wa malipo anakuta amelipwa siku 3 au 4 pekee bila maelezo yoyote.

Mbaya zaidi, hakuna karatasi mpya anayoletewa kuonyesha kuwa kiwango chake kimebadilishwa wala kupewa nafasi ya kusaini kuthibitisha kuwa anakubaliana na malipo hayo mapya yaliyopunguzwa. Hali hii inaleta maumivu makubwa kwa wafanyakazi kwa sababu wanakuwa wamefanya kazi halali, wamethibitishwa, lakini mwisho wa siku wanalipwa chini ya kiwango walichostahili bila uwazi wowote.

Pia kuna wakati watumishi wanalipwa fedha ambazo hawajawahi hata kusaini uthibitisho wake. Hali hii inakatisha tamaa na kuonyesha kuwa stahiki za watumishi hazipewi kipaumbele kinachostahili, jambo linalotushangaza sana ukizingatia mzigo mkubwa wa kazi tunaoubeba kila siku kutokana na upungufu wa watumishi hospitalini.

Vilevile, changamoto ni kubwa zaidi kwenye safari za rufaa za wagonjwa. Mfano, mtumishi anaweza kuondoka Kitete RRH saa 11 jioni akiwa amemsafirisha mgonjwa kwenda Mwanza, lakini posho anayopatiwa ni shilingi elfu 20 tu. Fedha hiyo hiyo anatakiwa aitumie kwa chakula, malazi ya kupumzika kabla ya kuanza safari ya kurudi Tabora pamoja na mahitaji mengine muhimu ya safari.

Kiuhalisia kiwango hicho hakitoshi kabisa ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi na gharama za maisha zilizopo sasa.

Tunapodai haki zetu tunaambiwa hospitali inaendesha miradi mingi na fedha hazitoshi, ilhali ukweli ni kwamba watumishi ni wachache na tunalazimika kufanya kazi kwa muda wa ziada ili kuhakikisha huduma kwa wananchi zinaendelea bila kusimama.

Tunaomba mamlaka husika zisikie kilio chetu na kuchukua hatua stahiki ili watumishi walipwe haki zao kwa wakati, kwa usahihi, kwa uwazi, na kwa kuzingatia uhalisia wa kazi wanazozifanya kila siku kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania.
 
Ni kweli hospital inakusanya mapato kwa wingi lakini sisi watumishi tunadai stahiki zetu kwa muda mrefu tu hatulipwi extra duty na call allowance tangu 2024, 2025 na 2026.

Ikitokea zimelipwa ni malipo ya mwenzi mmoja na mingine unayobakia hatulipwi, tukidai wanasema madeni yetu yapo wizarani.

Tuna hali mbali Viongozi tatueni changamoto hii na sio Maneno ya siasa tu, hali hii imefanya utendaji wa watumishi kua mbaya miaka na miaka
Hapo mchawi ni RRHMT, pesa ipo wanalipana wao kwa wao
 
Back
Top Bottom