A
Anonymous
Guest
Watumishi wa kada ya uhandisi walioajiriwa tarehe 1 Desemba 2020 katika shule za sekondari za ufundi za serikali wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa katika utumishi wa umma kutokana na kutopatiwa barua za ajira wala kuthibitishwa kazini kwa takribani miaka sita sasa.
Tatizo hilo linadaiwa kusababishwa na kutotambuliwa rasmi na Tume ya Utumishi wa Walimu, ambayo ina jukumu la kutoa barua za ajira na kuthibitisha watumishi kazini. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya watumishi hao walilazimika kuomba kuhamia katika taasisi nyingine zinazolingana na taaluma zao.
Hata hivyo, walipofika katika taasisi hizo, walielekezwa kuwa kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi, barua za ajira na uthibitisho wa ajira zinapaswa kutolewa na mwajiri wao wa kwanza. Hali hiyo imewalazimu kurejea katika halmashauri walikoanzia kazi kwa ajili ya kufuatilia nyaraka hizo.
Licha ya jitihada hizo, baadhi ya halmashauri zimekuwa zikikataa kuwahudumia kwa madai kuwa si watumishi wao tena. Mfano mmoja wapo ni Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Kutokana na changamoto hiyo, watumishi hao wanasema wanaendelea kupitia hali ngumu na sintofahamu kuhusu hatima yao katika utumishi wa umma. Tunaziomba mamlaka husika kutoa ufafanuzi na hatua za haraka ili kumaliza tatizo hilo.