Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Watumishi sita wa Bohari ya Dawa (MSD) akiwemo Mhasibu Mwandamizi na Wafamasia wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka 37 yakiwemo ya wizi wa dawa na vifaatiba vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.537, mali ya MSD.
Pia, washtakiwa hao kwa makusudi wanadaiwa kuisababishia MSD hasara ya Tsh. Bilioni 14.6.
Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7833 ni Mhasibu Mwandamizi, Suddi Abas (34), mkazi wa Kibamba Shule.
Wengine ambao wote ni wafamasia ni Petro Mdegela (42), mkazi wa Manga Veta; Rashid Hassan (34) na mkazi wa Isyesye.
Pia yupo, Edward Tengulaga (40), mkazi wa Manga Veta; Mfamasia wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, mkoani Songwe, Jackson Mahagi (39) na Wema Mohamed (39) ambaye ni mfamasia wa Wilaya ya Singida na mkazi wa Mandewa.
Watumishi hao wanadaiwa pia kutakatisha fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 5.537 kwa kununua mashamba, viwanja, gari, kujenga nyumba za kuishi na zingine za kupangisha, kuanzisha kampuni ya usafirishaji, kufungua duka la vifaa ya ujenzi pamoja na kufungua maduka ya dawa.
Chanzo: Mwananchi