Watumishi wa afya matatani tuhuma za rushwa, Shinyanga

Watumishi wa afya matatani tuhuma za rushwa, Shinyanga

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Watumishi wawili wa kada ya afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga (Nindo), akiwemo daktari mmoja na muuguzi mmoja, wamepewa onyo kali na kuagizwa kuhamishwa vituo vya kazi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na ukiukwaji wa maadili ya kazi.

Hatua hiyo imetangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, wakati akizungumza na watumishi wa kada ya afya wilayani humo ambapo asema uhamisho wa watumishi hao unalenga kupisha uchunguzi wa kina dhidi yao, kufuatia malalamiko ya kupokea fedha kutoka kwa wagonjwa nje ya mfumo rasmi wa malipo sambamba na kutumia lugha isiyofaa kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kuhakikisha watumishi wanaolalamikiwa wanahamishwa mara moja huku TAKUKURU ikipewa maelekezo ya kuingia kazini na kuendesha uchunguzi wa tuhuma hizo.

Aidha, DC Julius Mtatiro, amekemea vikali tabia ya baadhi ya madaktari kuwanyima wagonjwa dawa zilizopo hospitalini na badala yake kuwatuma kununua dawa katika maduka binafsi, akieleza kuwa kitendo hicho ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma na kinawaumiza wananchi.




Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom