KERO Watumishi wa halmashauri ya Nachingwea tunapitia changamoto nyingi ikiwemo kucheleweshewa posho za vikao

KERO Watumishi wa halmashauri ya Nachingwea tunapitia changamoto nyingi ikiwemo kucheleweshewa posho za vikao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea tunapitia kipindi kigumu kutokana na kucheleweshwa kwa stahiki zetu mbalimbali, hususan malipo ya posho za kuhudhuria vikao. Tatizo kubwa linalolalamikiwa ni kwamba Mkurugenzi wa Fedha (DT) amekuwa hapitishi malipo hayo kwa wakati.

Kuna watumishi ambao tayari wamehudhuria vikao vitatu hadi vinne lakini hadi sasa hawajalipwa stahiki zao. Hali hii imewakatisha tamaa na kuwafanya baadhi yao kushindwa kushiriki vikao vingine kwa sababu wanatumia fedha zao binafsi bila kurejeshewa.

Aidha, kumekuwa na malalamiko kuhusu mwenendo wa DT katika kuwahudumia watumishi. Inadaiwa kuwa mara nyingi amekuwa akitoa kauli zisizo za kiutumishi na zisizo rafiki kwa watumishi wanaofika ofisini kwake kufuatilia stahiki zao au wanapotekeleza majukumu yao, ikiwemo wale wanaotoka idara nyingine. Hali hiyo imejenga mazingira ya hofu na kuwafanya watumishi wengi kusita kufika ofisini kwake hata wanapokuwa na masuala ya kikazi yanayohitaji ushirikiano wake.

Vilevile, ucheleweshaji wa kutoa vibali vya matumizi (OC) kwa idara mbalimbali umeathiri utekelezaji wa shughuli za kila siku, na kusababisha baadhi ya idara kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Tunaziomba mamlaka husika kuchunguza kwa kina malalamiko haya na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha watumishi wanalipwa stahiki zao kwa wakati, wanapata huduma kwa heshima na weledi, na wanafanya kazi katika mazingira yanayozingatia misingi ya utumishi wa umma. Hali ya sasa imeendelea kushusha morali ya watumishi na kuathiri utendaji wa kazi katika halmashauri.
 
Nilitoa kero yangu ya DT wa halmashauri ya nachingwea kuhusu maswala ya fedha pamoja na kauli zisizo rafiki,, please nakuomba kero yangu uitume kwenye jukwaa la Instagram naamin huu ujumbe utafika sehemu husika nakuomba Sana tafadhali🙏🙏
 
Back
Top Bottom