Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Injili ya kale ya akina Petro ilikuwa rhema.
Rhema ni neno la Mungu kwa wakati husika. Yaani Mungu anasema kwa kinywa cha mtu. Anaweza kutumia neno hili la kila siku (logos) ila anaposema Mungu mwenyewe hulitia uzima na kutimiza kusudi lake kwa haraka kama umeme.
Ndio maana ukisoma kitabu cha Matendo ya mitume kimejaa matendo makuu mpaka kitabu kikaitwa "Matendo ya Mitume" na si mausia au maneno ya mitume.
Anania na Safira walipofanya udanganyifu, Petro alitamka neno "rhema" na ikawa vivyohivyo.
Sasa hivi, wewe hata ukipeleka sadaka pesa uliyofanya ujambazi, sawa, ulifanya ukahaba, sawa.
Neno kutoka kwa BWANA (rhema) halipo.
Sasa hivi, mtu akiuza mafuta ya upako, hata kahaba anamuuzia tu, hakuna shida, maana ni biashara kama biashara zingine.
Mafundisho yanayofundishwa makanisani sasa ni mepesi na ya kawaida. Mtu yeyote anayeweza kuongea anaweza kuhubiri bila wasiwasi.
Unaangalia tu nini kinatrendi kwa sasa, unalinganisha na maandiko ya kwenye Biblia, unashangiliwa, mchezo umeisha.
Wale wahubiri ambao hawasimami madhabahuni kuhubiri mpaka wasikie sauti ya Mungu ikiwaambia waseme nini, sasa hawapo.
Ni mazoea tu. Mtu akikumbuka niliwahi kufundisha somo fulani, nilipata credit, basi atalibeba akafundishe mahali pengine.
Kanisa limegeuka mahali pa kuanzisha vikundi vya kusaidiana na vya kikabila.
Mungu aliponye kanisa.
Muhubiri anapitia YouTube mahubiri ya wahubiri wengine, naye huyabeba kanisani kwake.
Iko wapi kazi ya Roho wa Mungu?
Watu wametengana kwa dhambi ya uzinzi, mpaka sasa wameona hakuna namna uzinzi usiwe dhambi ya kutengana, maana kanisa zima limejaa uzinzi.
Kanisa ambalo halina "NENO HAI" (rhema) ni kichaka cha uzinzi, uchawi, majungu, na kila aina ya dhambi.
Note: Watumishi wa Mungu wenye kujitoa kwa kila hali wapo, wanaotembea na Mungu kila leo wapo, ingawa ni wachache na si maarufu, wengi wao.
Video hii 👇👇 ni ya kuburudisha Uzi, haina undugu na mada hii