Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

Watumishi wa Mungu wamekuwa wakame rohoni sasa makanisani wanafundisha falsafa za kidunia, Falsafa ambazo unaweza kuzipata popote

A
Injili ya kale ya akina Petro ilikuwa rhema.

Rhema ni neno la Mungu kwa wakati husika. Yaani Mungu anasema kwa kinywa cha mtu. Anaweza kutumia neno hili la kila siku (logos) ila anaposema Mungu mwenyewe hulitia uzima na kutimiza kusudi lake kwa haraka kama umeme.

Ndio maana ukisoma kitabu cha Matendo ya mitume kimejaa matendo makuu mpaka kitabu kikaitwa "Matendo ya Mitume" na si mausia au maneno ya mitume.

Anania na Safira walipofanya udanganyifu, Petro alitamka neno "rhema" na ikawa vivyohivyo.

Sasa hivi, wewe hata ukipeleka sadaka pesa uliyofanya ujambazi, sawa, ulifanya ukahaba, sawa.

Neno kutoka kwa BWANA (rhema) halipo.

Sasa hivi, mtu akiuza mafuta ya upako, hata kahaba anamuuzia tu, hakuna shida, maana ni biashara kama biashara zingine.

Mafundisho yanayofundishwa makanisani sasa ni mepesi na ya kawaida. Mtu yeyote anayeweza kuongea anaweza kuhubiri bila wasiwasi.

Unaangalia tu nini kinatrendi kwa sasa, unalinganisha na maandiko ya kwenye Biblia, unashangiliwa, mchezo umeisha.

Wale wahubiri ambao hawasimami madhabahuni kuhubiri mpaka wasikie sauti ya Mungu ikiwaambia waseme nini, sasa hawapo.

Ni mazoea tu. Mtu akikumbuka niliwahi kufundisha somo fulani, nilipata credit, basi atalibeba akafundishe mahali pengine.

Kanisa limegeuka mahali pa kuanzisha vikundi vya kusaidiana na vya kikabila.

Mungu aliponye kanisa.

Muhubiri anapitia YouTube mahubiri ya wahubiri wengine, naye huyabeba kanisani kwake.

Iko wapi kazi ya Roho wa Mungu?

Watu wametengana kwa dhambi ya uzinzi, mpaka sasa wameona hakuna namna uzinzi usiwe dhambi ya kutengana, maana kanisa zima limejaa uzinzi.

Kanisa ambalo halina "NENO HAI" (rhema) ni kichaka cha uzinzi, uchawi, majungu, na kila aina ya dhambi.

Note: Watumishi wa Mungu wenye kujitoa kwa kila hali wapo, wanaotembea na Mungu kila leo wapo, ingawa ni wachache na si maarufu, wengi wao.
Video hii 👇👇 ni ya kuburudisha Uzi, haina undugu na mada hii
View attachment 2719692
Aisee!
 
Wakihubiri habari za wokovu na uzima wa milele mnawasema wachungaji wamepitwa na wakati na hata kanisani hamuendi, wakihubiri mambo mnayopenda kusikia mnasema wachungaji wamekengeuka kwani binadamu mnatakaje ninyi? mihemko na unafiki tu.
Nakazia hapo...Wachungaji Wakifanya miujiza na ishara mnasema Miujiza fake hichi kizazi Cha Instagram hata ufanye nini watakukosoa tu
 
Kanisa limejengwa juu ya mitume na manabii

Kama tunataka kurudisha kanisa (mwili wa kisiri wa Yesu Kristo) kama vile lilivyotenda kazi katika kitabu cha Matendo ya Mitume Basi turudi kwenye basics zile zile walizokuwa nazo mitume kwa sababu yeye Mungu hana kigeugeu (Malaki 3) Yesu Kristo ni yeye yule Jana Leo na hata milele (Ebr 13:8)

Mungu akija Leo hatauhukumu ulimwengu kwa taratibu/mapokeo/kanuni za Imani za kikatoliki,kilutheri,kipentekoste, Methodist, Anglican, Baptist,Kisabato,mashahidi wa Yehova etc

Ulimwengu ukihukumiwa kwa mapokeo ya kilutheri basi Wote tumeangamia, ukihukumiwa kwa mapokeo na kanuni za Kisabato basi wengine wote tumekwisha.

Mungu atauhukumu ulimwengu kwa Neno lake (Mbingu na Nchi zitapita ila hilo Neno halitopita)

Turudi basi kwenye basics za Matendo ya Mitume (sio kwa mihemuko) namna walivyobatiza, namna walivyomhubiri Kristo.

Kwa sababu Mkuu wa wajenzi Paulo aliuweka msingi na akasema kwenye Wagalatia 1:8 (ikiwa malaika kutoka Mbinguni au mtu mwingine yeyote atawahubiri injili nyingine tofauti na hii niliyohubiri na alaaniwe)

Bible mwishoni imetoa onyo ukiongeza au ukipunguza jina lako linaondolewa kwenye kitabu cha uzima,na mapigo utapata.

Turudi kwenye basics za kanisa la kwanza la kibibilia sio tasfiri za watu walizojiwekea creeds (kanuni za imani) and Dogmas (mafundisho ya sharti)

Asanteni.
Waefeso 2:20-22

Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi.

Umenena Vyema Mkuu
 
Ni kweli makanisa yamejisahau, hayakemei dhambi tena.

Yanachotaka ni sadaka tu bila kutaka kujua imetoka wapi, iwe imetokana na umalaya, ujambazi n.k

Makanisa hayana Aibu tena wala hofu ya Mungu
 
Nyakati za mwisho,matetemeko,njaa,vita kila mahali,mabadiliko ya tabia Nchi!Muyaonapo hayo shangilieni huku mkijua saa ya hukumu ipo karibu!
😂😂😂😂😂Acha ujinga wewe....hamna mda katika historia ambapo hivi vitu havipo...so dunia ingeishaga mda tu...kuwa na akili na wewe bac...eti njaa
 
Back
Top Bottom