Angalia Msukuma anavyowashambuliaga Wakurugenzi kule Jimboni kwake. Yaani Mwanasiasa yeyote akitaka kujitoa kwenye kutowajibika basi huanza kumshambulia Mtumishi wa Umma anayehusika na jambo Fulani.
Musukuma kwa kupitia Kamati inayohusika na zabuni angeweza kuzuia kile alichodai ni matumizi mabaya ya fedha za Covid lakini akajinyamazia tu na kusubiria ashambulie.
Tabia hii imekuwepo sana, anagalia juzi Ali Hapi alichofanya mbele ya Mheshimiwa Rais. Yaani always watumishi wa umma wamekuwa ni watu wa kusukumiziwa kila aina ya uozo - kuonwa wazembe, wabadhirifu, wajeuri, nk. Ilmradi tu mwanasiasa aonekanae yeye ni mfuatiliaji au ni mtendaji.
Sio kwamba watumishi wa umma wenye tabia hizo hawapo lakini wanasiasa wamezidi sana kuwasukumizia watumishi kwa makusudi kuwa wanawajibika na mauozo kama hayo.
Wanasiasa sasa wanavyojipendelea. Wao wakichaguliwa au kuteuliwa siku inayofuata huapishwa na kuanza kula maposho kede kede. Mwanasiasa akimaliza muda wake haichukui hata muda wa Mwezi mmoja kulipwa pensheni zake.
Sasa njoo kwa Mtumishi wa umma huku - akiajiriwa hata kulipwa fedha za kujikimu kwa wakati wakati ameanza kazi hamna na wengine hawajawahi hata kulipwa.
Ukipandishwa cheo ndiyo mpaka usubirie bajeti ipite eti ndiyo ulipwe. Ukiomba uhamisho utasubiria hata mwaka mzima. Ukiomba ruhusu hivyo hivyo. Ukistaafu ndiyo basi tena hayo malipo yako ya pensheni yanakuijia tayari upo choka mbaya.
Jamani jamani, wanasiasa muwe basi na huruma. Ninyi mnakula sana manono ya nchi hii, basi achene basi hata kuwapakazia tu watumishi wa umma ilimradi tu nyie mpate sifa kupitia mipakazo hiyo!