voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,935
Naona kila jumba bovu mnamtumia mwendazake....Tabia hii imekomaa sana kipindi cha mwenda zake na bahati mbaya wanaomshauri mama hawamwambii ukweli. Huko Halmashauri wale wakurugenzi walikuwa wanatokana na wakuu wa idara na huwa na uelewa mkubwa wa masuala ya kiutendaji. Mwendazake akateua wakurugenzi toka chama watu wasiojua chochote kile.
1. Ni makosa raisi kuteua mkurugenzi na mkuu wa wilaya au mkoa uwajibikaji unapotea na sio sababu ya madudu ya kutafuna pesa na miradi kutokamilika. Miaka ya kabla ya sasa katibu mkuu utumishi alikuwa akiteua wakurugenzi mambo yalikuwa Safi.
2. Wakurugenzi ni watumishi wa umma hivyo wale wenye sifa na uzoefu wa ukuu wa idara wateuliwe ukurugenzi sio UVCCM na makada wa chama hawa hawana wanalojua na kuna siku watasababisha hasara kubwa sana.
Akhsante
Kama vipi si umfuate huko aliko ukamalizane nae?
Huwezi kuwatetea wezi wa mali na kodi za maskini eti kisa utawala bora.......
Je huo utawala bora unaruhusu ukwapuaji na kujitajirisha kwa njia zisizo halali?
Wenzetu nchi zingine wanasoma sheria ili ziwasaidie wao na jamii zao.
Tofauti na Tanzania ambapo vijana wanasoma ili waje kuwa wezi wa kodi za wazazi wao.
Mwanasheria anafanya ubia na Polisi ili kumkamua mteja wake au kuutumia mwanya wa uwakili na kujimilikisha mali za mteja.
Mifano ni mingi na huo wa Geita ni mmojawapo.
Kwanza tujiulize...mkurugenzi wa halmashauri ana umuhimu gani na wa kipekee wa kumfanya astahili hizo staha za bei ghari namna hiyo?
Wizi mtupu!