Huyu Mama ni mmoja kati ya walioongea jana mbele ya PM. Alidaiwa kodi ya Tsh 30 Billion kwa containers zake 10 alizo import. Baada ya kuonyesha kuwa hana hizo fedha akatengenezewa mashtaka ya uhujumu uchumi. Waliosokia kikao cha PM wakamfutia shtaka la uhujumu uchumi. Na kisha usiku wa kuamkia mkutano wa PM wakamuita akatoe mzigo.
Hivi ni vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wafanyabiashara na nchi kwa ujumla. Nashauri vyombo vya dola vishughulike na Meneja TRA wa Mkoa wa Ilala pale Kipata na wengine wote waliohusika
View attachment 2626036
Hakika hao TRA wanastahiri kinachowahusu.
Lakini hapo hapo, huyo mama ni sehemu muhimu wa tatizo lenyewe.
Huyu ni mfanya biashara mzoefu, hadi kapata uwezo wa kuingiza kontena zote hizo, ni wazi anao uzoefu kwenye kazi hiyo.
Sasa swali la kujiuliza ni, je, alipoagiza hakujua kwamba mzigo wake ungehitaji kulipiwa ushuru stahiki?
Inavyoonekana, alishakuwa na uzoefu wa njia za mkato, kwa njia moja au nyingine, safari hii kakuta mtu wake hayupo, na waliokuwepo wakaona fursa yao kumtoa upepo.
Haya ndiyo madudu yanayotakiwa kuondolewa kwenye mfumo mzima wa kodi.
Pasiwepo na mtu yeyote kujitungia tu taratibu zake pembeni.
Taratibu zilizopo zifuatwe na ziimarishwe zaidi ili zifanye kazi ipasavyo.
Kodi ya "kukadiriwa na mtu" bila ya mwongozo wa kufanya hivyo unaoeleweka ndiyo njia ya kuvuruga kazi za TRA.