Watumishi wa TRA Waliochaji Rushwa ya Tsh 30 Billion, Kisha Kumfungulia Huyu Mama Kesi ya Uhujumu Uchumi, Washughulikiwe

Watumishi wa TRA Waliochaji Rushwa ya Tsh 30 Billion, Kisha Kumfungulia Huyu Mama Kesi ya Uhujumu Uchumi, Washughulikiwe

Kwenye magari? Inawezekana ila haijanitokea. Anyway kama ipo basi imepungua sana tofauti na kipindi cha ukaguzi wa kutumia macho.
Shukuru Mungu kama haijakutokea, ile wanayoongeza tofauti na calculator ya TRA inatoka wapi? Mbona inakuwa haina maelezo ya ziada, iweje calculator inataka ulipe 3mln lkn yeye atoe asesiment ya 3.8mln ?
 
Huyu Mama ni mmoja kati ya walioongea jana mbele ya PM. Alidaiwa kodi ya Tsh 30 Billion kwa containers zake 10 alizo import. Baada ya kuonyesha kuwa hana hizo fedha akatengenezewa mashtaka ya uhujumu uchumi. Waliosokia kikao cha PM wakamfutia shtaka la uhujumu uchumi. Na kisha usiku wa kuamkia mkutano wa PM wakamuita akatoe mzigo.

Hivi ni vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wafanyabiashara na nchi kwa ujumla. Nashauri vyombo vya dola vishughulike na Meneja TRA wa Mkoa wa Ilala pale Kipata na wengine wote waliohusika
View attachment 2626036
Umesikikiza upande mmoja tu, hata wao ni wezi, wakwepa kodi na magendo usiseme.
Wafanyabiashara na tra wote wezi tu
 
Ni miaka mitano sio miwili, mitano kwenda nyuma kuanzia siku aliyotoa tamko hilo.

Japo Rais hana mamlaka kusimama jukwaani kufuta kodi! Ukimpa Rais au watendaji wa umma mamlaka ya kufuta kodi kwa mdomo basi mmewapa pia mamlaka ya kutunga kodi kwa mdomo!

Hawa marais wakiwa nyumbani kwao huwa wanatucheka sana tulivyo mambumbumbu wa dunia, yani tunamwongezea kiongozi madaraka ya mdomo ambayo kimakaratasi hana! Ndio maana maafisa wa TRA wanawaambia wafanyabiashara amri za majukwaani ni kauli za uongo, hadaa za wanasiasa.

Kwa hiyo, kwa tamaduni za kodi za Tanzania, ukikwepa kodi miaka miwili mpaka mitano, deni linaenda linapotezewa kwa huruma ya Rais mpya! Biashara ikikushinda kwa kodi achana nayo fanya mengine baadae ibuka tena itakuwa imesamehewa, ndio hicho Samia alichonuia kuki encourage ??? Hakuna nchi inayoendeshwa hivyo!

Tunalalamika tunataka Katiba Mpya ya kupunguza mamlaka ya Rais wakati huo huo tunampa madaraka ambayo hata kwenye Katiba ya sasa hana!
Kwa comments hizi wewe ni mfanyakazi wa TRA tu nyinyi ndiyo mnakusanya rushwa kwa kubambikiza wafanyabiashara kodi za kutisha.
 
...hii nchi bila kutoa Demo viongozi wasimamizi wakuu wa utendaji kila siku haya yatatokea...Dawa hapo ni kukamata Meneja mkoa na watendaji wake wanaomfuatia kama wa 3 kuwafukuza kazi ,kuwafungulia kesi na kuwasweka ndani miaka hata 10 ili wao na familia zao zionje joto la jiwe la unyanyasaji wa watu kwenye uchumi wao...Viongozi wengine kupitia hao watajifunza kusimamia sekta/idara na sio kukaa ofisini na kuzunguka na kiti, kunywa chai zenye virutubisho kila muda wakiwa wanasikilizia safari za wizarani na kusubiri kuletewa taarifa na walio chini yao sio wao kuingia field, Mzee Magufuli(RIP) muda mwingine alikuwa sahihi sana,alikuwa hacheki na Kima Kwenye ujinga kama huu.
 
Ujue hata Sheria mbovu ni chanzo Cha rushwa na kuwatajirisha TRA officers,maana masheria mengine hayana applicability kiuhalisia ndio mwisho mtu kukwepa hyo Kodi anaona awape rushwa ma officer ili asilipe.
Pia fine za hovyo Kwa kosa dogo mfano la receipt labda ya laki moja huku fine milion Tano huoni kuwa huyo mfanyabiashara ataamua atoe tu rushwa kulipo kulipa fine.
Sheria mbovu ndio zinachangia rushwa isiishe nchini, plus too much bureaucracy kwenye ma office ya umma.

Nchi imemshinda mama wa unguja.
2025 utatambua uhalisia

Hili la serikali kutafuta pesa kwa mabavu sio kitu kigeni, Kodi ni kitu ambacho lazima kiwepo na inataka uaminifu mkubwa wa kimalaika na Kama motisha RIP Mkapa aliongeza mshahara ya watu wa TRA ili tu kushawishi waache kudai rushwa lakini Bahati mbaya ikawa ni kichocheo cha rushwa, tujiulize kidogo ni Nani anayemsimamia TRA na kumwacha mpaka anakuwa na kiburi? Nina I anayemsimamia waziri wa fedha na anamwacha mpaka anatukana wabunge wenzie? Ni Nani anayemsimamia waziri wa viwanda na biashara? Mwisho niseme tu kuwa Prof Assad CAG mtiifu alijaribu kutuonyesha njia lakini bado hatutaki kutoa tongotongo zetu ili tuone na kumkabili adui namba moja BUNGE ambaye ameshindwa kumsimamia SERIKALI
 
Na container 20 unazichukuliaje yani ?

Hakuna mali inayojaza container 20 yenye thamani ya bilioni 20 za kodi ?

Mfanyabiashara mwenyewe kasema alipotajiwa hiyo kodi akasema hana hela, hakusema kodi imekosewa, kasema sikuwa na hela. What does that mean? Anajua kilichomo. Na si ajabu kodi hiyo ni cummulative assesment ya biashara ya miaka 10 bila kulipa kodi. Hii ni hadithi ya majukwaani ya upande mmoja. Huwezi kufanya conclusion yeyote kwa kihadithi cha dakika mbili cha upande mmoja.
We ni mjinga container moja la Vitenge la 40
Ft Kodi yake Kwa Bandar ya Dar ni tsh , milion 240 Hadi 300.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Huyu Mama ni mmoja kati ya walioongea jana mbele ya PM. Alidaiwa kodi ya Tsh 30 Billion kwa containers zake 10 alizo import. Baada ya kuonyesha kuwa hana hizo fedha akatengenezewa mashtaka ya uhujumu uchumi. Waliosokia kikao cha PM wakamfutia shtaka la uhujumu uchumi. Na kisha usiku wa kuamkia mkutano wa PM wakamuita akatoe mzigo.

Hivi ni vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya wafanyabiashara na nchi kwa ujumla. Nashauri vyombo vya dola vishughulike na Meneja TRA wa Mkoa wa Ilala pale Kipata na wengine wote waliohusika
View attachment 2626036
Tykumvuke pia waTz wanakipata chance ya kukusagia kunguni wanasaga kweli.

Mahakaman unahitajika ushahid wa kutosha mkuu.

Lipeni KODI , haya mazingira ya rushwa hata watoaji wanayapenda
 
We ni mjinga container moja la Vitenge la 40
Ft Kodi yake Kwa Bandar ya Dar ni tsh , milion 240 Hadi 300.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app

TRA wamekwambia ni container za vitenge tupu ?

Na kwa nini aliwaambia sina hela sijauza badala ya kusema hiyo kodi sio sahihi ?

Na ilikuwaje hakulipa kodi ya bandarini na kuja kukamatiwa nchi kavu. baada ya kufanyiwa investigation, aliyapitishaje huko bandarini ?

We unabugia tu story ya upande mmoja ya jukwaani kama kichwa cha mtoto kinavyopokea hadithi ya sungura na fisi? What a chucklehead.
 
Tatizo ni Sheria zetu zimewafanya Polisi na TRA kuwa miungu watu.Mamlaka kuu ingepewa mahakama kama ilivyo kwa wenzetu haya marushwa yangepungua
 
Msikilize vizuri. Hajasema aliombwa rushwa ya bilion 30. Na hajatamka neno rushwa. Huyu mleta mada wetu ndio ame introduce rushwa.
Tafsiri yake ni hiyo, yaani rushwa..

Kodi ndio ilikuwa bilioni 30. Amesema "TRA wakatoa assessment ya bilioni 30." Assessment maana yake kodi, sio rushwa. Makadirio ya kodi.
Bado tafsiri ya hiyo assessment Ina uelekeo wa rushwa tena bila hata kuwa na diploma ya "uta - KUKURU!!"

Kuna maswali muhimu kadhaa ya kujiuliza ni hili;

1. Ikawaje wakatengeneza njama za kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi na wao wenyewe tena kuifuta/ondoa mahakamani kesi hiyo?. Jibu ni rahisi: Kum - indimidate atishike ili wapate wanachokitaka!!

2. Na unadhani ikawaje variation ya hiyo assessment ikawa inabadilika kiwango kutoka 30b kisha 15b and then 10b na mwisho "njoo uchukue mzigo wako?"

##Unataka ufundishwe na nani ili ujue kuwa hiyo ni direct rushwa na hata kama zingetoka zisingeingia ktk fuko la serikali??
Mfanyabiashara ndio anajua ndani ya makontena 20 kulikuwa na nini.
It doesn't matter.

Ingekuwa ni bidhaa isiyoruhusiwa ishu hapo isingekuwa Kodi tena bali ni kosa la jinai. Kwa hiyo walipaswa kumshitaki tu mfanyabiashara

Hizo zilikuwa ni bidhaa za kawaida tu lakini eti Kodi 30bn. Hata Tanzania Breweries LTD (TBL) au Bakhresa Group of Companies LTD hawalipi kodi ya kiwango hicho tena Kwa mwaka mzima!!
Na ndio maana wala hakubisha kiasi cha kodi, yeye kasema "sikuwa na hela."

Hakuwa na hela hiyo ya rushwa kwa kiwango hicho...!!

Kumbuka kuwa, kama business woman, lazima alikuwa na pesa ya kulipa Kodi halali ya serikali..!!

Ni mfanyabiashara gani makini anaweza kuagiza bidhaa ya biashara yake asiweke na bajeti ya Kodi, tozo na ushuru wa serikali..??
She knows what she brung to the country. Ni hadithi ya upande mmoja wa mfanyabiashara. Hatujasikia claims za TRA.
Katika scenario ya namna hii, you don't need to hear anything from TRA Kwa sababu picha ya rushwa iko very crystal clear.!!

Yaani mfumo wa rushwa ktk nchi hii unaundwa na syndicate hatari sana ikihusisha vigogo toka Kila idara muhimu serikalini: TRA, polisi, TISS, WIZARA ya fedha na pengine mpaka ikulu..
 
Back
Top Bottom