Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Kuna tangazo linazunguka juu ya kutolipwa mishahara kwa wafanyakazi wa umma ambao walichukua fomu za kuomba kupata ridhaa kutokak chama cha mapinduzi ili wapeperushe bendera ya kuwania nafasi za ubunge.

Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma...
Unaijuwa katiba ya Tanzania ya mwaka 1977?
 
Zipo taarifa za kuzuia mishahara ya watumishi waliogombea nafasi mbalimbali katika mwezi huu wa Julai, aliyetoa ushauri huu ana nia ya kutaka kumuharibia Rais Magufuli 2020, Oktoba 28.

Rais Magufuli nikuombe uingilie kati hili, si jambo la afya na ukingazatia watia nia hao wataombwa kwenda kusaidia kuweka umoja katika majimbo waliogombea, nani atakubali kwenda kusaidia chama wakati mshahara wake ulikatwa...
Kwani si ndio sheria inavyotaka au ni tamko tu? Nadhani ni sheria, sina uhakika lakini ninachokumbuka sheria iko wazi na waraka wa kukumbusha ulitolewa. Makonda mwezi huu hana mshahara
 
Zipo taarifa za kuzuia mishahara ya watumishi waliogombea nafasi mbalimbali katika mwezi huu wa Julai, aliyetoa ushauri huu ana nia ya kutaka kumuharibia Rais Magufuli 2020, Oktoba 28.

Rais Magufuli nikuombe uingilie kati hili, si jambo la afya na ukingazatia watia nia hao wataombwa kwenda kusaidia kuweka umoja katika majimbo waliogombea, nani atakubali kwenda kusaidia chama wakati mshahara wake ulikatwa...

Wakatwe tuu mishahara. Unaacha wanafunzi darasani unaenda mitaani huko kusaka kura halafu unataka mshahara. Kwa kazi gani?
 
Wakatwe tuu mishahara.. Unaacha wanafunzi darasani unaenda mitaani huko kusaka kura halafu unataka mshahara. Kwa kazi gani??
Nisaidie mbinu watakayoitumia kuwapata hao watumishi bila kuwaonea
 
Sina shaka na huo waraka au hiyo Sheria ya uchaguzi. Hoja yangu ni: WATATUMIA MBINU GANI KUJUWA HUYU ALICHUKUA FOMU, AKAJAZA NA AKARUDISHA?

Ni hilo tu
 
hivi kwa nini haswa binaadamu unakuwa na roho mbaya dhidi ya binaadamu mwenzio asipate haki yake ya mshahara na wakati anategemewa na familia?!hii sio sawa, tusiwe hivyo maana unapo zuia mshahara wake maana yake watoto wake wasile!

Jamani hebu punguzeni kuwa na roho za kikatili dhidi ya binaadaamu mwenzio
 
*WAHAMIAJI HARAMU.*

1) Maulid Mtulia 🛠
2) Abdallah Mtolea 🛠
3) Peter Lijualikali 🛠
4) David Silinde 🛠
5) Joshua Nassari 🛠
6) Patrobas Katambi 🛠
7) Paulina Gekul 🛠
8) Kalist Lazaro 🛠
9) Albert Msando 🛠
10) Elia Michael 🛠️
11) Kalanga 🛠
12) Mashinji 🛠
14) Mwambe 🛠
15) Marwa Ryoba🛠
 
Waraka Namba 1 wa Utumishi wa Umma wa 2015 unamtaka mtumishi kabla hajaenda kugombea cheo cha kisiasa aombe (na apewe) likizo ya bila malipo. Kipindi hicho chote hatalipwa mshahara! Akipitishwa na kamati kuu/NEC anakoma utumishi wa umma.

Watu tumesaini na kula hivi viapo halafu sasa tunajifanya kusahau
 
Duhh... Mbona noma sasa hii Mkuu.
Balaa sio dogo... lakini hili jambo ni kweli. Mara ya kwanza nilijua ni mshahara tu wa July, lakini habari za uhakika kutoka kwenye chanzo changu zinadai, WAMEFUKUZWA kabisa na barua walizopewa ni za kuwaondoa kwenye payroll.

Sijui kuhusu utaratibu gani utatumika ku-justify lakini ndio hivyo tena.
 
Nafikiri hao ni watakao fuzu kura za maoni..

Wegi wamesharejea makazini.
 
Waliomba ruhusa pia majina yao yapo

Magufuli kaamua kufuata sheria!!!lakni ni Wenda wazimu unaomba ruhusa ya wiki moja na unajisemelea kuwa unaenda kutia nia!!!
kule kwetu RUNGWE MBEYA kuna Afisa alienda kutia nia kwao Mbinga,hili tamko nadhani limemtoa kijasho!!
 
Sina shaka na huo waraka au hiyo Sheria ya uchaguzi.
Hoja yangu ni: WATATUMIA MBINU GANI KUJUWA HUYU ALICHUKUA FOMU, AKAJAZA NA AKARUDISHA?
Ni hilo tu
Mbona hata wakija JF wataona hata waliopata kura 0 (sifuri). Aidha makatibu wamikoa wa CCM wataonesha hata kura za watiania
 
Waraka Namba 1 wa Utumishi wa Umma wa 2015 unamtaka mtumishi kabla hajaenda kugombea cheo cha kisiasa aombe (na apewe) likizo ya bila malipo. Kipindi hicho chote hatalipwa mshahara! Akipitishwa na kamati kuu/NEC anakoma utumishi wa umma.

Watu tumesaini na kula hivi viapo halafu sasa tunajifanya kusahau
Asante mama, humu watu wa kulaumu kila jambo hadi wanakataa kuwa huwa hawaendi choo
 
Kupanga ni kuchagua,

Kwenye maisha unaweza kuamua kuwa mtumishi wa uma au kufanya shughuli binafsi,

Ukiamua kuingia kwenye siasa unapaswa kuachana na maswala ya utumishi wa uma, kuchanganya haya kunaleta mgogano wa kimaslahi.
 
Kibinadamu sio sawa kabisa, kisheria ni sawa kwa kuwa anayelipwa ni yule aliyefanya Kazi,.
Sasa kama karibu mwezi huu wote mtumishi alikuwa kwenye kampeni atalipwa vipi.?
 
Back
Top Bottom