Watumishi wa umma wamkumbuka Rais Magufuli kuwa na hofu juu ya mishahara kucheleweshwa

Watumishi wa umma wamkumbuka Rais Magufuli kuwa na hofu juu ya mishahara kucheleweshwa

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Imeelezwa kwa watumishi wa umma toka maeneo mbali mbali wameanza kumkumbuka Hayati Magufuli kuhusu mishahara yao kucheleweshwa na utawala wa sasa.

Wanadai kuwa enzo za hayati Magufuli walikua wakipokea mishahara yao kuanzia tarehe 2, 22 au 23 ikichelewa sana. Lakini kwa mfano mwezi huu hadi leo tarehe 24/5/2021 bado hawajapokea chochote.

Wanachodai ni kwamba pamoja na kidogo alichowapa Magufuli lakini kilikuwa kinatoka kwa wakati. Wanahoji kua ikiwa mtu ulimpatia mshahara wake tarehe 23 mwezi uliopita halafu leo unampa tarehe 24 maana yake umezidisha mwezi na ni kwanini?

Wanaingizwa na hofu kwa mifumo ya Serikali kuanza kuchezewa na watu wachache ambao hawamuogopi Mama yetu hali ya hofu itakayopelekea kucheleweshwa kwa mishahara yao zaidi huko mbeleni.

Katika hili ninamshauri Rais wetu msikivu Mama Samia na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu wawe wakali sana kuepusha madhara huko mbeleni.
 
Hizi ndio akili zetu watanzania. Unafiki mwanzo mwisho.

Mshahara wa January 2021 ulitoka January 25. Rais alikuwa alikuwa Nani?

Na pia mshahara wa December 2020 ulitoka Dec 22 je kutoka Dec 22 mpaka January 25 zilizidishwa siku ngapi?

Serikali haipo Kwa ajili ya watumishi wa umma pekee.
 
Back
Top Bottom