peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Sasa ni dhahiri kuwa mshahara wa July 2021 watumishi wataupokea August 2021.Imeelezwa kwa watumishi wa umma toka maeneo mbali mbali wameanza kumkumbuka Hayati Magufuli kuhusu mishahara yao kucheleweshwa na utawala wa sasa. Wanadai kua enzo za hayati Magufuli walikua wakipokea mishahara yao kuanzia tarehe 21,22 au 23 ikichelewa sana. Lakini kwa mfano mwezi huu hadi leo tarehe 24/5/2021 bado hawajapokea chochote.
Wanachodai ni kwamba pamoja na kidogo alichowapa Magufuli lakini kilikua kinatoka kwa wakati. Wanahoji kua ikiwa mtu ulimpatia mshahara wake tarehe 23 mwezi uliopita halafu leo unampa tarehe 24 maana yake umezidisha mwezi na ni kwanini?
Wanaingizwa na hofu kwa mifumo ya serikali kuanza kuchezewa na watu wachache ambao hawamuogopi Mama yetu hali ya hofu itakayopelekea kucheleweshwa kwa mishahara yao zaidi huko mbeleni.
Katika hili ninamshauri Rais wetu msikivu Mama Samia na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu wawe wakali sana kuepusha madhara huko mbeleni.