Watumishi wa umma wamkumbuka Rais Magufuli kuwa na hofu juu ya mishahara kucheleweshwa

Sasa ni dhahiri kuwa mshahara wa July 2021 watumishi wataupokea August 2021.
 
Acha use'ngerema basi... Sukuma gang kwenye uchawa pro Max+
 
Inanikumbusha wakati Mose anawatoa waisrael utumwani misri,walipofika jangwani wakawa na kiu na njaa. Wakaanza kumlaumu Mose kuwa heri angewaacha utumwani ili wale na kushiba kuliko adha walopata!
 
Mishahara imetoka leo.sijui unataka nini mkuu.
 
Hata mtoto anahaki yake Kwa wazazi wake, Ila ikitokea haki hiyo imechelewa kuipewa, haiondoi kuwa wao ni wazazi wake, na haiondoi ukweli Kwamba, bado haki ni yake na ataipata hata ikicheleweshwa!

Na kingine, ni Kwamba, kila serikali na mtindo wake wa kushughurikia mambo hata kama ni kwa kujivutavuta, ila ndio kushughurikia
 
We msukuma ndo unaona hiyo kadhia, sie wengine hatuwezi kumkumbuka mwendazake, alale pema peponi
 
Mataga uliyekubuhu, nani amilie muuaji Jiwe, Potelea mbali wacha tukae na njaa lkn tuna uhuru, hatutekwi, hatupotei , hatubambikiwa kesi. Acha lifilie kwa mbali lioze
 
Wee! kata huo mdomo paka pilipili.
Tunaomba tusijepata mtu kama huyo tena wewe unasema tunamkumbuka????
We siyo mtanzania hakika.
 
Wewe ni muongo! Hivyo uache pia kutusemea kwa uongo. Tarehe 22 ilikuwa ni Jumamosi, hivyo isingekuwa rahisi kwa Serikali kuingiza mshahara. Leo Jumatatu mshahara umeingia!

Mataga acheni kuilazimisha Legacy ya Hayati! Hakuna Mtumishi wa umma mwenye akili anaweza kumkumbuka Hayati Magufuli kwa mazuri! Na huu ndiyo ukweli mchungu kwenu.
 
Acha uongo wako mtumishi gani anaemkumbuka mtu aliyemkomoa
 
Kitu kishasoma , wengine washaukomba wote na wameshapiga hadi salary advance
 
Watumishi wa Umma wa Zambia.
 
Wewe unayemkumbuka mfuate kaburini Chato. Pia wewe si mwajiriwa unapalilia uteuzi kinakuuma nini! Unataka kutukopa?
Mama Samia Hoyee. CCM Hoyee, huyu mama ana akili nyingi! Amewanunua CHADEMA wote bila kutumia hela! Wapinzani wote wa Magufuli, sasa ni CCM wapya! CHADEMA wanademkana na CCM kujipendekeza kwa mama. Rais Samia hoyee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…