Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Kwani kulikuwa kuna haja ya kumtukana huyo mtu? Nani punguani sasa, kati yake na yako?
 
Kiondolewe ili ufiche nini?.
 
Acha tu wapigane na ukuta.Marekebisho ni lazima.
 
Kitu kama hicho hakikuwepo rasmi katika kada ya utumishi wa umma. Swala la ibada lipo siku zote aliingiliani na kusajili makabila au dini. Hata Nyerere alikataa kuwatambua watu kwa kabila au imani ya mtu.
Kuna watu wamefanya serikalini mpaka wanatoka hauwezi fahamu kabila au imani yao. Swala la mazishi imani haihusiani na serikali, hilo uachiwa ndugu au ukoo.
Tusitetee mambo tu kwa upambe. Nampenda Rais Samia, ila kwa hili alikemee.

Kusema kuna maeneo hawana break ni uongo ati kisa wakristo wengi. Toka miaka enzi za Nyerere nakumbuka Ijumaa ilikuwa ni ruksa kwa ajili ya waislam kufanya ibada.

Tuliosoma wakati huo tukiwa wadogo. Watu shuleni walidanganya wakichelewa au wakitaka pumzika unaaga tu wenda ibada. Hakuna alie zuiwa.
Zamani Jumamosi ilikuwa nusu siku ikaamuliwa kuwa siku ya mapumziko bila kuuliza watu dini zao, hii ilikuwa kwa wasabato.
Serikalini hakuna anae lazimishwa fanya kazi wakati anaibada. Najua baadhi ya ofisi zimeandaa mahala pa swala kwa waislamu maeneo ya kazi.
Na wapo ikifika wakati wa ibada wanaenda kuswali hakuna anae katazwa.
Hili swala halina tija yoyote.
 
Huyu maza nashauri vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi viwe vinamkalisha daily kwa lazima kumsikilizisha hotuba za Mzee wetu baba wa Taifa Nan vitupe mrejesho clip anazomaliza.nchi sasa ishamshinda
 
Asante mkuu!.
 
Makafiri kwenye ubora wenu, ila tulisha wajua hila zenu hamtusumbui kipindi cha mwendazake kulikuwa na namba kubwa ya makafiri lkn kwasababu waislaam tumejaliwa subra tukakaa kimya kuimba kupokezana mbwaa nyieee!!
Tena koko.[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Naona sie wa VIJIWENI tumekazana kujadili kwani WATUMISHI WENYEWE WA UMMA WANASEMAJE
 
We soma tu chet chako, pia hata hii km huna dini utajaza mpagani

Hakuna cheti cha kuzaliwa kinachoonesha kabila na dini.

Nani amekuambia mpagani hana dini? By definition, a pagan is a person holding religious beliefs other than those of the main world religions!
 
Nimependa substance na uandishi wako,hasa jinsi ulivyoweza ku-express hisia zako kwenye maandishi.Hongera sana.Umenikumbusha Mwalimu Nyerere alivyokuwa anaongea.
 
Tupe na Tawimu za Samia pia mapendekezo yenu mnatakaje

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Inasemekana Hawa wenye umri mrefu ndiyo huwapangia vifo wenzao

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.
 
Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?
 
Mkuu sio tu kwa watumishi wa hazina, hiyo ni kwa watumishi wote wa serikali. Labda wanataka kujenga makanisa na misikiti mahali pa kazi.
 
Very disappointing!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…