Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?
Mimi nauliza tu, kwani dini ni kristo na uislamu tu? Kuna hindu, sikh, bahai na kadhalika.
 
sijui hio form ila nashangaa mbona ni miaka ming particulars huwa kuna sehem ya tribe, religion ni muda mrefu kweli lipi limekua la ajabu
 
Data is power

Watu hawataki dini zao zijulikane, wanataka kuficha nini?

Iacheni serikali ipate takwimu sahihi ili kama kuna ubaguzi wa kidini katika ajira iweze kurekebisha hilo tatizo kwa ajili ya umoja na mshikamano wa kitaifa
 
Mgalitaya amechanganyikiwa. Ndio mambo mkuu Keki ya Taifa ni ya wote
 
Upuuzi wa mama.
Habari wana JF ..

Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.

Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.

Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!

Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.

Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......

Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.

Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.

Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?

KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!

Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.

Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,

 
Mungu aliipenda Sana Tz kwa kutupa Nyerere kua baba wa Taifa maana bila hivyo nchi hii ingekua imegawanyika kikabila/kidini mbaya kabisa.

Asante Sana Mungu.
Na tusipo ungana kukataa kwa nguvu viashiria vya kutugawa kuna siku tutalia na kusaga meno
 
ivi kweli hiki ni kitu kipya???? mbona watanzania tuna lawama sanaaa..... mbona hizo ni taarifa za kawaida sanaaa tena baadhi ya watumishi huzijaza kila mwisho wa mwaka...

ulivyoandika ni kana kwamba hata huko shuleni ulikopitia hukuwahi kuliona hili... tena hadi vikundi vipo, huko maofisini mna hadi makundi ya kikabila

BADILIKA sio kila kitu Raisi, Raisi.....

ulisema hutakosoa so ishu zingine zote zinazoendelea kwako ni sawa ni hii ndo imekuumuza????
Kwamba hadi gesiti hausi huu utaratibu upo tokea kitambo
 
sijui hio form ila nashangaa mbona ni miaka ming particulars huwa kuna sehem ya tribe, religion ni muda mrefu kweli lipi limekua la ajabu
Haya mambo yanaanzia jikoni, huenda walioyavujisha wanajua kinachoendelea ndio maana wanalalamika...
 
Kipolisi nadhani kuulizwa kuhusu kabila kuna justification.

Kisheria, kwenye defences to criminal liability kuna defence moja inaitwa 'PROVOCATION' au KUGAFIRISHWA kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rsmi sana. Huu ni utetezi unaoweza kumsaidia mtuhumiwa kupewa adhabu ndogo Mahakamani au kuachiwa huru kabisa kutokana na kabila lake TU.

Ngoja nikupe mfano wa defence hii, ukimfumania mkeo/mumeo kitandani kwenu (matrimonial bed) anachakatana na mwanamke/mwanaume mwingine ukapandwa na hasira ukamjeruhi, hapa utakua umekuwa provoked Kisheria kwasababu ya kupandwa na hasira (heat of passion); hasira ambayo inatofautiana kati ya kabila na kabila au mtu na mtu.

Inaaminika Wakurya wana hasira kali na za haraka tofauti na wasukuma labda, ingawa wakati mwingine unaweza kukuta ni kinyume chake kwa kumkuta mkurya mpole lakini pia unaweza kukutana na msukuma mtata, hii itategemea na jinsi Mahakama itakavyopima.

Ninachotaka kusema ni kwamba kabila tu linaweza kukusaidia ukaachiwa huru kwa kuaminika kwamba watu wa kabila flani wana hasira za karibu.

Lakini hata kwenye kesi za ndoa kama talaka, kwa mfano kwenye ishu ya custody of children, kabla Mahakama haijaamua mtoto/watoto wakaishi na baba au mama, moja ya criteria ni kuangalia MILA NA DESTURI ZA KABILA HUSIKA, kwamba kwa kawaida wanandoa wanapoachana ni nani (baba au mama) anayestahili kubakia na watoto.

Naomba kubakia.

Hoja ya kishamba zilizokwisha pitwa na wakati
 
Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.

Sidhani Kama Samia anaijua vizuri historia ya nchi anayoingoza kwani kama angeijua hii leo asingekuwa anavalishwa ngozi za wanyama na kuushabikia Uchifu nchini!!
Nyerere alitoka ukoo wa Chief wa wazanaki na hata hivyo alifanikiwa kupigachini uchifu kwasababu alijua kwa undani kuwa hiyo taasisi haileti umoja katika nchi bali kuigawa nchi!! Umoja wa nchi hii umewezeshwa pamoja na mambo mengine kwa kuutokomeza ukabila hivyo Hangaya kuwapigia chepuo hao machifu wa zamani ni kutaka kuligawa TAIFA!! Mama jitahidi kusoma historia ya nchi ili angalau upate kuifahamu ingawa hujajaliwa kuvitembelea vijiji vingi hapa nchini!!!
 
Mi naona hakuna shida yoyote hivo vitu kuulizwa kwani sio vyako hivo vilivyoulizwa? Kuna ubaya gani mwajiri kukufahamu vizuri mtumishi wake?
 
Back
Top Bottom