Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi taarifa za mzazi kwenye CV zinakazi gani?Habari wana JF ..
Mimi niliahidi sitamkosoa Rais Samia, kwa sababu nilishawakosoa sana ma Rais wa nchi hii hadi nachoka; lakini Kuna mambo ni mazito huwezi hata kufikiri yanaweza kufanyika kwa karne hii.
Mimi niwaombe Serikali, niwaombe CCM, niwaombe washauri wa Rais, kama mmechoka, mtuachie hili Taifa.
Wengine bado tunataka kuliona Taifa letu likiwa moja.
Vyombo vya usalama, basi mshaurini mheshimiwa Rais vizuri, msijisahau sana mkaiacha nchi kwenye auto-pilot.
Niwakumbusheni Taifa hili halikujengwa kwa matofali, la hasha!
Mpitisheni Mh. Rais katika historia ndogo ndogo zile njema, zilizotufanya Watanzania japo tukawa wamoja, potelea pote na umaskini wetu.
Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......
Zipo taarifa zingine, za kipuuzi zinazoombwa, ila haina haja sana kuzitaja, kwani hazina athari sana kama hizi mbili.
Hivi kweli, leo mnataka DINI ya mtumishi, iwasaidie nini?
Hii taarifa mnaitumia kuboresha nini?
Udini wa nini katika Tz ya leo.
Tuna ajenda gani na Dini za watu, (watumishi). DINI, DINI.....DINI...!!!!?....,leo tunauliza DINI yako ni ipi? Kweli mh. Rais Samia.
Halafu mnataka na KABILA, kabila la mtumishi litumike kuboresha nini?
Mna ajenda gani huko?
KABILA, leo mnamuuliza mtu KABILA. Kweli mh Rais Samia , ulisema wewe huna kabila, sijui ni Mzanzibar, sasa hawa watumishi, karne ya 21, mwaka 2022, wawajazie makabila yao, muyajue, myafanyie nini?!
Mh Rais Samia, hebu kataa mambo mengine.
Siku Taifa hili likiparaganyika mikononi mwako, hao unaowaona, watakukataa.
Mfumo wa CV (format) na taarifa zinazotakiwa nimeambatanisha hapa.
denooJ , MTAZAMO , barafu , Tindo , Chige , shige2 , Malcolm X5 , MALCOM LUMUMBA ,
Tujenge nchi yetu sisi sote kwa pamoja, tushirikiane kwa pamojaKichuguu,
Hizo takwimu hapo chini zinatoka katika Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania.
Uliwekwa kwa madhumuni ya kuwazindua Watanzania hali iliyoko nchini:
''Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani Mwaka (2015), Rais alifanya uteuzi wa Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi mbalimbali. Uteuzi wake ulikuwa kama ifuatavyo:
Mawaziri na Manaibu: 30.
Waislamu 10, sawa na asilimia 33%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 67%.
Makatibu Wakuu na Manaibu: 50.
Waislamu 10, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 40, sawa na asilimia 80%.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya: 166.
Waislamu 41, sawa na asilimia 25%.
Wakristo 125, sawa na asilimia 75%.
Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya: 163.
Waislamu 24, sawa na asilimia 15%.
Wakristo 139, sawa na asilimia 85%.
Wakurugenzi mbalimbali: 249.
Waislamu 45, sawa na asilimia 18%.
Wakristo 204, sawa na asilimia 82%.
Manaibu Kamishna wa Polisi: 25.
Waislamu 5, sawa na asilimia 20%.
Wakristo 20, sawa na asilimia 80%.
Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi: 33
Waislamu 7, sawa na asilimia 21%.
Wakristo 26, sawa na asilimia 79%.
Jumla Kuu ya Uteuzi:
Waislamu asilimia 20%.
Wakristo asilimia 80%.
Uteuzi huo umekuwa kama Sera kwa teuzi zinazoendelea ndani ya miaka yote mitano. Vilevile kama Mwongozo kwa wateule wenye mamlaka ya kuteuwa. Mwelekeo huo unakinzana na Katiba ya nchi ibara ya 13(4)(5), inayokataza ubaguzi wa aina zote. Kwa hakika Taifa halihitaji kiongozi wa nchi akiwa Muislamu basi ateuwe idadi kubwa ya Waislamu wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi au akiwa Mkristo atumie uongozi wake kuteua idadi kubwa ya Wakristo wenzake katika uongozi nchini. Au akiwa Mzanaki ateuwe idadi kubwa ya Wazanaki wenzake katika nafasi mbalimbali za uongozi na mfano wa hayo.''
Basi hayo yameanza hivi karibuni tu. Mimi niliulizwa dini wakati wa kuanza darasa la kwanza miaka ya sitini kwa vile kulikuwa na kipindi cha dini kwenye mtaala. baada ya hapo sijawahi kuu;lizwa dini yangu mahala popote nilipofanya kazi, iwe ni kwenye mashirika ya umma, serikalini hadi nilipoingia kwenye elimu ya juu. Kwanza sikuwa mfuasi wa dini, bali jina tu kwani kwenye ukoo wetu kuna mkusanyiko wa dini mbalimbaliJidanganye, sehemu nyingi suala la dini na kabila hujitokeza. Taasisi kubwa kabisa yenye kudai taarifa za dini ni elimu ya msingi na kuendelea, mgonjwa hospitali, ukikamatwa na polisi, mhimili wa bunge n.k.
Inawezekana ikaileweka vibaya kwasababu tayar Kuna mitizamo tofauti juu ya Kiongozi mkuu.
Ila hili jambo lipo na lilikuwepo kwa watumishi. Kuna muda watu walihoji na majibu yalionyesha ni kwa nia njema, Mfano mtumishi anapofariki zipo taratibu za kumhifadhi kiimani kabla ndugu zake hawajapatikana au kufika eneo husika, lakini pia kulikuwepo na mgongano wa nyakat za ibada hasa kwa Wasabato na Waislam.
Kuna maeneo ijumaa hawana break kabisa kwakuwa idadi kubwa ya wakaazi ni Wakristo kwahiyo hili la kuwatambua inaeezekana halina sura ya udini au ukabila.
Fisadi mwenyewe mnataka kupendelena. Kazi zipatikane kwa Credit si kwa kabila wala dini. Period!Waliozoea kunufaika na mfumo kristo nawaona povu kama lote! Tulieni dawa iwaingie mafisadi nyie.
Kwenye rekodi za serikali huwa hakuna dini wala kabila la mtu. Nyerere aliondoa hiyo zamani sana wakati taifa bado ni changa, na hata marais waislamu Mwinyi na Kikwete hawakuirudisha.
Sasa tumepata mwislamu kamili ndiye anayeyaleta. Katika teuzi wake naona kipengele cha dini kimekuwa ni cha muhimu sana kwake; na ili kukihalalisha ndiyo maana ameunganisha na ukabila akianzia na kurudisha uchifu.
View attachment 2095774
Imekula kwenu Wazee wa Mfumo Kristo. Mama hapendi dhulma haki bin haki. Tulieni dawa iwaingie.Fisadi mwenyewe mnataka kupendelena. Kazi zipatikane kwa Credit si kwa kabila wala dini. Period!
Hapana siwazi hivyo. Nawaza hivi, kwanza nikuulize - je! Unajua kitu kinacho itwa affirmative action? Mimi sijui kiswahili chake. Tanzania tume wahi kufanya kitu hicho. Kilifanyika hivi : Mikoa au sehemu zilizo kuwa zime endelea kielimu, pass mark ya kuingia sekondary ilikuwa kubwa kuliko mikoa/sehemu zile ambazo elimu ilikuwa haijapewa kipaumbele. Mfano pass mark ya Bukoba ilikuwa juu kuliko ya Ngara au Mara. Ikapelekea hata kukuta mchaga au Mhaya anaitwa Wambura, Chacha, Ndimugwanko etc. Maana wasomi hao walihamia sehemu zenye pass mark za chini kwa mtihani uleule.Kwa hiyo unaamini huu ni mkakati maalumu?
Mfano mkigundua Wakristo ni wengi, mnaanza kubana wao wasiingie kazini, muweke Dini zingine?
Au kama waislamu ni wengi, wazuiwe kuajiriwa, hata kama wao ndio wana sifa zaidi za kielimu, kimafunzo, kiutendaji. Unawaza hivyo?!
Wakristo wenzangu tuache chuki mbona Wakati wa mkatoliki mwenzetu hatukua na haya maneno ya uzushi?Na mkome!
Nchi inafunguliwa
Achana nae huyo, yeye ndiyo mdini na mkabila. Kwenye mikataba ya ajira hivyo vipengele vya dini na kabila vyote vipoBoss sio kweli mm wakati naanza ajira kuna kipengele kwenye mkataba wangu ajira za serikali kinauliza dini.Hili jambo sio jipya nashangaa kuona mleta mada analikuza kana kwamba limekuja leo.Au kwakuwa kwenye ajira za serikali ni mgeni.
Sasa kwa nini upate hofu?Hakuna kitu kinachoitwa 'mfumo kristu' kwenye hili taifa........hizo ni kampeni za kueneza chuki, fitina na hila ovu dhidi ya kundi fulani la ki-imani.
Ina maana watu makazini hawajuani dini zao? Kujua dini ya mwenzako mbona ni rahisi Sana hususani ukiwa unafanya nae kazi sehemu moja!!? Hivi ninyi mpo tanzania hiihii? Watu tunafanya kazi pamoja tunajuana dini mpaka makabila, unaweza ukawa na rafiki wa dini tofauti na wewe ukawaacha wa dini na kabila lako mbona kawaida Sana.Mama Samoa Luna watu wanamwangusha technically
Hizo fomu hicho kipengele cha dini na kabila kiondolewe
In hatari sababu kitawapa watu mianya ya kuoendeleana mfano bosi was Shirika au wizara akijua huyu dini yangu au kabila langu ataibua upendeleo hata kwenye ajira MTU anayeajiri aweza kitumia kuonea wengine kuwa ah huyu anayeomba kazi in kabila language akampendelea
Hayo yalikuwa yameondolewa naona yanarudishwa lengo nini?
Hata kwenye sensa yaliondolewa kuwa MTU asihojiwe kabila au dini yake .Waislamu siasa Kali walitaka kiwemo ili serikali iwasaidie kujua wako wangapi .Wakajibiwa nendeni mkajihesabu huko misikitini
Sasa naona serikali imeanza sensa ya kuhesabu waislamu wako wangapi
Hiyo mifomu yenye dini na kabila ilishaondolewa hiyo sehemu za ajira huyu mama anataka kuturudisha nyuma