Hahahaaa,
Mh Lisu, Kura yangu huipati, na Kura yangu Mimi yeyote atakayeikosa huwa no kama laana vile, ni lazima Kwanza ashindwe kwenye ngazi yoyote Ile
Pili, umaarufu wake unaishia hapohapo na hawezi tena kuja kuwa kiongozi mkubwa ktk nchi hii
Zaidi ya huruma ya anayekuwa kiongozi wa nchi, ama amteue ktk ngazi Fulani au kumpa ubalozi!
Sikupi si Kwa sababu nakuchukia" hapana, sikupi Kwa sababu umerudi ukiwa hueleweki kabisa
Umerudi ukiwa kama si Mtanzania Mwenzetu, umerudi ukiwa umebeba mambo moyoni mwako ambayo ndiyo yanayotupa wasiwasi mwingi Sisi waona mbali
Na kitendo cha mataifa yasiyokuwa na utamaduni na Mila za kistarabu kuwa nyuma yako, ndio kabisa...yanazidi kutufanya tukuogope
Kuna kila Dalili za wewe ukiwa Raisi wetu, Tukaanza kuambiwa, vitu Fulani tunaweza kuvigusa na kuvitumia Ila vitu Fulani na Fulani haturuhusiwi kuvigusa, Kwa kuwa tukivigusa twaweza kufa""
Ingawa Sisi ni huru, na rasilimali zote ni zetu
Amri hizi za kama kipindi cha Adamu na hawa Edeni, ni kama tunaziona Sana moyoni mwako