Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 3,474
- 3,744
Kuna tetesi ambazo hazijakanushwa kwamba watumishi waliostaafu kazi hawajalipwa pesa zao na mifuko ya hifadhi ya jamii km nssf na PSPF. Tetesi hizo zinasema kuwa mifuko hii haina fedha na hali yake ni mbaya, inasemekana akiba za wafanyakazi kwa kiwango kikubwa zimechotwa na serikali ya wanyonge ya CCM na kupangiwa matumizi mengine bila kupangiwa bajeti na bunge la JMT.
Ni vema CCM na serikali yake km kweli ilichota akiba hizi za wafanyakazi kuzirejesha na kuwalipa wazee hawa kwani ni jasho lao na wamelitumikia taifa hili kwa miaka 60. Kuendelea kuwazungusha inaonyesha Serikali eidha haina pesa ama ina lengo wastaafu hawa wafe na familia zao kuja kudhurumiwa. Tunasoma mapato yameongezeka uchumi unakua kwa kasi kwanini wasilipwe visenti vyao.
Siku zote mnafiki hana rafiki.