Kuna mdogo wangu mmoja yupo Finland huu ni mwezi wa saba unakatika toka emeenda. Huko keshafanya kazi mbii na hii aliyonayo ni ya tatu toka amefika, japo si kazi za maana wala si za kuitumia nguvu au akili sana lakini ana uhakika wa kusave $1300 to 1700 kwa mwezi. Hiyo ni saving tu baada ya kulipa bills zote na mahitaji yake muhimu keshamaliza. Tatizo la huyu dogo anadai amepamiss sana nyumbani bongo hususani chakula na mahusiano na watu, anadai Finland hana marafiki wengi zaidi ya girlfriend aliyempata two months ago. So anasema anataka kurudi bongo kuja kukomaa na life ya huku hivyo hivyo, yeye akishapata mtaji inamtosha. Na mimi ninachokifanya kila nikisoma threads za kusikitisha na kukatisha tamaa kama hizi basi huwa nakopi then naziforwad kwake kupitia WhatsApp au email yake ili kumtahadharisha kinachoendelea bongo ikiwezekana asahau kabisa kurudi huku. Lengo langu sio kumtisha bali kumpa angalizo kuwa Bongo Bahati Mbaya.
NB: Kwa wale walio nje ya nchi au wenye ndugu nje ya nchi na maisha yao yanaenda vizuri kiasi kwamba anaweza kumbuka kutumia ndugu zake hata $ 400 na kuendelea kwa mwezi, pls tuendelee kuwakatisha tamaa za kurudi bongo hata iweje. Ni bora kuwa mtumwa nchi ya watu kuliko kuwa mtumwa katika nchi yako mwenyewe, inauma sana.