A
Anonymous
Guest
Watumishi wa ajira mpya wa Januari 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega (Nzega DC) bado hatujalipwa fedha za kujikimu hadi leo.
Kinachotushangaza ni kwamba baadhi ya watumishi, hususan wa Idara ya Afya, wamepokea sehemu ya fedha hizo, huku wengi wetu tukiendelea kusubiri bila kupata malipo yoyote. Tunapojaribu kufuatilia na kuuliza kuhusu suala hili, hatupewi majibu ya wazi wala maelezo yanayoridhisha.
Hali hii imekuwa ikituweka katika mazingira magumu ya kifedha, hasa kwa kuwa fedha za kujikimu ni muhimu kwa watumishi wapya wanapoanza kazi katika vituo vyao vya kazi.
Tunaomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi na kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha watumishi wote wanaostahili wanapata fedha zao za kujikimu kwa wakati.