KERO Watumishi wengi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi hatupati stahiki zetu, pia kuna mazingira ya upendeleo

KERO Watumishi wengi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi hatupati stahiki zetu, pia kuna mazingira ya upendeleo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimeona bora suala hili lifike kwenye mikono ya umma, kwani kuendelea kubaki kimya inamaanisha hali itakuwa ngumu na mazingira magumu ya kazi kwetu.

Watumishi wengi wa umma Moshi tunafanya kazi kwa kujituma lakini linapokuja suala la kupata stahiki zetu za kisheria kama posho, malipo ya muda wa ziada overtime, safari, na stahiki nyingine halali zilizo kwenye bajeti ni changamoto

Mbali na hapo kumekuwa na mazingira ya mfumo wa vitisho na ubaguzi wa wazi, hali hii si nzuri kwa kuwa inachangia ufanisi wetu kushuka.

Jambo lingine ni kuwa hata katika vikao vya ndani napo kumekuwa na mazingira ya vitisho na kiburi, baadhi tunatishwa hatuna cha kufanya.

Pia soma ~ Halmashauri ya Manispaa ya Moshi watumishi tunaoomba ruhusa ya kwenda kusoma huwa tunanyimwa bila sababu

Kuna migogoro kadhaa ya ndani ikiwemo kati ya Viongozi na Mabaraza ya Madiwani, kuthibitisha hilo kuna Waziri aliyekuja hivi karibuni alibaini hilo na kulisema ndani ya kikao cha ndani, alikuwa mkali sana na akasema angekuwa na uwezo katika nafasi ya kufanya mabadiliko angekuwa ameyafanya muda mrefu.

Unakuta Mtumishi anafanya kazi kwa uaminifu, anakusanya mapato ya halmashauri, lakini inapofika wakati wa kulipwa stahiki zake zilizopo kwenye bajeti, anaambiwa hakuna fedha na anatishiwa kufukuzwa kazi. Hivi hapo tunajenga au tunabomoa?

Tunatoa rai kwa Mamlaka za Juu, TAMISEMI na Mkoa wa Kilimanjaro kuingilia kati kwa haraka.
 
Maisha ni magumu jamani wafanyie kazi haya malalamiko haya yanaposhindwa kufanyiwa kazi yanaongeza hasira kwa wananchi
 
Back
Top Bottom