Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Nikiwa kwenye utumishi wa umma kwa miaka karibu 8 sasa nina experience ya kutosha kuhusu utumishi na maisha ya utumishi.
Kama mlinzi msomi mwenye shahada ya HRM nimefanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha kuwa watumishi wa umma % kubwa wanakwenda kazini huku kichwani wamebeba mawazo ya wizi wa mali za umma, wizi wa pesa za umma, rushwa na udokozi sehemu za kazi.
Ukiona mtumishi wa umma anaishi maisha duni basi jua kuwa huyo aidha hapendi tabia za wizi au hana fursa ya kuiba au kupata rushwa sehemu yake ya kazi.
Serikali isipochukua hatua kudhibiti rushwa na wizi makazini basi isahau kuhusu maendeleo.
Huu upigaji dili huanza kwa wakurugenzi mpaka kwetu sisi huku chini. Unatamani upambane lakini unakuja kugundua kuwa utapambana na wenye nguvu basi unaungana nao kula mema ya nchi ili nawe upeleke watoto shule za gari za njano.