wankuru nyankuru
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 495
- 775
Mimi ni mmoja wa watumishi wa Serikali tuliobainika kuwa na vyeti feki kwenye zoezi la uhakiki wa vyeti feki lililofanyika mwaka 2016.
Nakumbuka takribani watumishi 9000 tulikumbwa na hili sakata la kuwa na vyeti feki. Kwa tathimini iliyofanyika kupitia kundi la sogosi la watumishi tuliokutwa na vyeti feki mwaka 2016 inaonesha kuwa zaidi ya 80% ya watumishi hao waliokutwa na vyeti feki hawana kinyongo na mgombea urais kupitia CCM na wanadai kuwa wangetamani watumishi wenzao waliokutwa na vyeti feki wamuunge mkono mgombea kupitia CCM ili aendelee kuinyoosha nchi iliyokuwa imeoza kwa masuala ya ufisadi, janja janja kwa baadhi ya vigogo waliokuwa wanatumia nafasi zao kuwaingiza ndugu zao serikalini bila kufuata taratibu za Serikali.
Wakaenda mbali kwa kusema na kukiri kuwa in kweli waliwazibia nafasi za ajira serikalini watoto wa maskini waliosoma lakini hawakupata ajira Serikalini kutokana na sababu za baadhi ya wahuni kuziba nafasi.
Kufuatia mjadala unaondelea huko kwenye kundi la sogosi wengi ( majority) wanatoa maoni kuwa watamchagua Magufuli tarehe 28/10/2020 ili aendelee kuinyoosha nchi.
Wengine pia wameomba watumishi ambao wanasema hawajapandishwa madaraja wasiwe na wasi wasi na wamuunge mkono Magufuli kwani tayari ameshaahidi kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara minono kabla kipindi chake kuisha.