Uchaguzi 2020 Watumishi wenzangu tuliotumbuliwa kwa sakata la vyeti feki tumchague Magufuli 2020

Hata kama mlitumbuliwa kwa vyeti feki, lakini wehuoni kwamba basi mlipaswa mlipwe stahiki zenu kwa utumishi wenu ulio tukuka kabla hamja tumbuliwa..??
Dhambi ni dhambi tu regardless dhambi ilibeba dhamira chanya lakn iliumiza wengi
 
W
Kwani waliokua na vyeti feki ni wahutu?au wanyarwanda?kipo wapi mbona hata kuajiri watu wapya hamna?tofautisha ukatili na kua strict,hebu niambie nchi imenufaika na kipi kwa kuwatumbua vyeti feki?
Hebu niambie nani alitengeneza hizo loop holes?natumai kuna chama kilitawala hapo katikati tofauti na CCM?natumai Hawa victims hawakufanya kazi na jitihada zao hazikujenga Taifa ,Natumai hili kosa wao wenyewe ndio waliifanya serikali i paralyse mifumo yake isifanye kazi ili wapate kazi ,natumai maelfu ya watendaji wa serikali hawakushiriki,natumai pia Hawa watu hawakua wanachangia mafao ya mfuko wa jamii ambayo serikali hukopaga ,na Nadhani pia serikali walikua hawakati paye as you earn bila kusahau hela hizi walikua wanatumia kenya ,Uganda,Rwanda au nje ya nchi wakiutengeneza uchumi wa huko

Hivi unafahamu serikali inaweza ikaanzisha program hata Kama haina faida ili mradi tu wapunguze unemployment rate na kuchochea uchumi?

Hamna sheria isiyokua na exception hapa ndio maana ya busara inakuja
Uwe mtanzania au mhutu, udanganyifu sehemu yoyote haukubaliki. Kama una mtoto wako anasoma msisitize asome kwa bidii, ili asije kulazimika kutengeneza vyeti feki Kama wewe.
 
Kwani report ya vyeti feki maraisi waliopita unadhani hawakupewa?busara mkuu na ndio maana kuna utofauti Kati ya kua katili na strict
 
wachache sana tulioelewa hiki kitu mimi kama muhakiki mwandishi kajaribu kuficha dhumuni lake kwa kutumia mtindo wa kupindua manene em someni tena kinyume chake mtapata jibu
 
Unalazimisha maji kupanda mlima, unapoteza muda wako.
 
Hata kama mlitumbuliwa kwa vyeti feki, lakini wehuoni kwamba basi mlipaswa mlipwe stahiki zenu kwa utumishi wenu ulio tukuka kabla hamja tumbuliwa..??
Wengi walifunguwa akaunti zao za bank baada kufukuzwa ili wakafe kabisa na njaa.
Hilo halioni
 
Mimi ni mmoja wa watumishi wa Serikali tuliobainika kuwa na vyeti feki kwenye zoezi la uhakiki wa vyeti feki lililofanyika mwaka 2016.

Nakumbuka takribani watumishi 9000 tulikumbwa na hili sakata la kuwa na vyeti feki. Kwa tathimini iliyofanyika kupitia kundi la sogosi la watumishi tuliokutwa na vyeti feki mwaka 2016 inaonesha kuwa zaidi ya 80% ya watumishi hao waliokutwa na vyeti feki hawana kinyongo na mgombea urais kupitia CCM na wanadai kuwa wangetamani watumishi wenzao waliokutwa na vyeti feki wamuunge mkono mgombea kupitia CCM ili aendelee kuinyoosha nchi iliyokuwa imeoza kwa masuala ya ufisadi, janja janja kwa baadhi ya vigogo waliokuwa wanatumia nafasi zao kuwaingiza ndugu zao serikalini bila kufuata taratibu za Serikali.

Wakaenda mbali kwa kusema na kukiri kuwa in kweli waliwazibia nafasi za ajira serikalini watoto wa maskini waliosoma lakini hawakupata ajira Serikalini kutokana na sababu za baadhi ya wahuni kuziba nafasi.

Kufuatia mjadala unaondelea huko kwenye kundi la sogosi wengi ( majority) wanatoa maoni kuwa watamchagua Magufuli tarehe 28/10/2020 ili aendelee kuinyoosha nchi.

Wengine pia wameomba watumishi ambao wanasema hawajapandishwa madaraja wasiwe na wasi wasi na wamuunge mkono Magufuli kwani tayari ameshaahidi kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara minono kabla kipindi chake kuisha.
CCM HATUHITAJI KURA ZA WAHUJUMU UCHUMII.
 
Kwani report ya vyeti feki maraisi waliopita unadhani hawakupewa?busara mkuu na ndio maana kuna utofauti Kati ya kua katili na strict
Kwahiyo ulitaka nchi uendelee kulea huo uozo?? Yaani tujihesabu tuna wasomi ilhali wasomi Ni wa kugushi😳? Busara ndo hizo, watu waumie, Ila huo ushenzi utoweke.
 
Kwani Jiwe anataka kura za wenye vyeti feki na familia zao ? Nazo SI Ni kura feki au? Sasa hivi ndio amewaona watu alifikiri akiwafukuza watakufa? Mbona wako hai ? Vipi na kura za wapiga diri nazo anazitaka ? Hajakwambia ?
 
HATUDANGANYIKI!
kuungama dhambi kwa padre na Mungu kuwa usamehewe kwa kutumia cheti feki kazini na kuwazibia wengine nafasi wenye vyeti halali kwa muhimu kuliko kushupaza shingo

Majuto ni kuungama na kumpa kura Magufuli. Usiopofanya hivyo huonyeshi Roho ya majuto na Mungu hawajibiki mbeleni kukusaidia wewe wala kizazi chako
 
Kwahiyo ulitaka nchi uendelee kulea huo uozo?? Yaani tujihesabu tuna wasomi ilhali wasomi Ni wa kugushi[emoji15]? Busara ndo hizo, watu waumie, Ila huo ushenzi utoweke.
Kuna maccm kama Polepole yana DHAMBI. Unafunga MIRIJA ya UCHUMI Nchi nzima. Wananchi wanalia NJA.

Wakisema vyuma vimekaza eti unawafunga badala kufungua mirija ya Uchumi.

Huu ujinga wote unafanywa ili uweze kuwaDHIBITI siku ya UCHAGUZI kwa kuwapa buku mbili wajaze viwanja.
 
kuungama dhambi kwa padre na Mungu kuwa usamehewe kwa kutumia cheti feki kazini na kuwazibia wengine nafasi wenye vyeti halali kwa muhimu kuliko kushupaza shingo

Majuto ni kuungama na kumpa kura Magufuli. Usiopofanya hivyo huonyeshi Roho ya majuto na Mungu hawajibiki mbeleni kukusaidia wewe wala kizazi chako
HATUDANGANYIKI!
 
Mimi ni mmoja wa watumishi wa Serikali tuliobainika kuwa na vyeti feki kwenye zoezi la uhakiki wa vyeti feki lililofanyika mwaka 2016.

Nakumbuka takribani watumishi 9000 tulikumbwa na hili sakata la kuwa na vyeti feki. Kwa tathimini iliyofanyika kupitia kundi la sogosi la watumishi tuliokutwa na vyeti feki mwaka 2016 inaonesha kuwa zaidi ya 80% ya watumishi hao waliokutwa na vyeti feki hawana kinyongo na mgombea urais kupitia CCM na wanadai kuwa wangetamani watumishi wenzao waliokutwa na vyeti feki wamuunge mkono mgombea kupitia CCM ili aendelee kuinyoosha nchi iliyokuwa imeoza kwa masuala ya ufisadi, janja janja kwa baadhi ya vigogo waliokuwa wanatumia nafasi zao kuwaingiza ndugu zao serikalini bila kufuata taratibu za Serikali.

Wakaenda mbali kwa kusema na kukiri kuwa in kweli waliwazibia nafasi za ajira serikalini watoto wa maskini waliosoma lakini hawakupata ajira Serikalini kutokana na sababu za baadhi ya wahuni kuziba nafasi.

Kufuatia mjadala unaondelea huko kwenye kundi la sogosi wengi ( majority) wanatoa maoni kuwa watamchagua Magufuli tarehe 28/10/2020 ili aendelee kuinyoosha nchi.

Wengine pia wameomba watumishi ambao wanasema hawajapandishwa madaraja wasiwe na wasi wasi na wamuunge mkono Magufuli kwani tayari ameshaahidi kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara minono kabla kipindi chake kuisha.
Tuovunjiwa nyumba zetu kupisha barabara tu comment wapi?
 
Back
Top Bottom