Uchaguzi 2020 Watumishi wenzangu tuliotumbuliwa kwa sakata la vyeti feki tumchague Magufuli 2020

Uchaguzi 2020 Watumishi wenzangu tuliotumbuliwa kwa sakata la vyeti feki tumchague Magufuli 2020

Hesabu zako sio halisia. Watumishi 9000×watoto wao×wenza wao×ndugu tegemezi wao× wasamaria wema= ...............

Hivyo kundi lenye hasira za watumishi kutimuliwa bila ingalau kulipwa mafao ni zaidi ya watumishi husika wenyewe
Adi namuonea huruma Msukum Wa watu..naamn uko alipo anajuta kwa iki alichokifanya
 
W
Uwe mtanzania au mhutu, udanganyifu sehemu yoyote haukubaliki. Kama una mtoto wako anasoma msisitize asome kwa bidii, ili asije kulazimika kutengeneza vyeti feki Kama wewe.
Ni kifungu namba ngap kinamzuia mtu aliyekutwa na hatia ya kughushi cheti asipate stahik zake baada ya kufukuzwa Kazi?..Ndio wamefukuzwa kaz ,sawa,ila kwann wamenyimwa adi mafao yao?
 
Kwaio pamoja na kutumbua huko walioajiriwa ni wangapi?
 
Ni kifungu namba ngap kinamzuia mtu aliyekutwa na hatia ya kughushi cheti asipate stahik zake baada ya kufukuzwa Kazi?..Ndio wamefukuzwa kaz ,sawa,ila kwann wamenyimwa adi mafao yao?
Kwanini, msishukuru kwamba serikali haikuwachukulia hatua zaidi baada ya kuwaachisha kazi, hao wajinga?
 
Ni kifungu namba ngap kinamzuia mtu aliyekutwa na hatia ya kughushi cheti asipate stahik zake baada ya kufukuzwa Kazi?..Ndio wamefukuzwa kaz ,sawa,ila kwann wamenyimwa adi mafao yao?
Kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu hujui ni kosa?
 
Kwahiyo ulitaka nchi uendelee kulea huo uozo?? Yaani tujihesabu tuna wasomi ilhali wasomi Ni wa kugushi[emoji15]? Busara ndo hizo, watu waumie, Ila huo ushenzi utoweke.
Ushenzi huo umetoweka pamoja na maelfu ya watu kuumia?
Hakuna vyeti feki maofisini?
Unataka tutoe orodha hapa?
 
Ungejua kutumbuliwa vyeti feki kunavyouma wala usingejifananisha nao
 
Ungejua kutumbuliwa vyeti feki kunavyouma wala usingejifananisha nao
Unajua maumivu waliyopata wenye vyeti halali waliokosa kazi au vyeo sababu ya nafasi zao kuzibwa na wenye vyeti feki?
 
Naomba nikuulize swali michango yetu kwenye mifuko ya hifadhi ipo wapi, kwa nn tusilipwe
 
Hata kama mlitumbuliwa kwa vyeti feki, lakini wehuoni kwamba basi mlipaswa mlipwe stahiki zenu kwa utumishi wenu ulio tukuka kabla hamja tumbuliwa..??
Hata wasipompigia kura bado JPM atashinda kwa kishindo
 
Inawezekana mleta mada yuko hapa?
Screenshot_20200921-051126.jpg
 
Kwa vyote vile hata wakipiga kura ya hapana kwake jumla yao ni 9000 unafikiri watamuondoa la hasha. Mimi nitampa kura ya ndiyo aendelee kudhibiti
Jumlisha na wake zao au waume zao na watoto wao na rafiki zao na watu wenye akili kidogo inayojitegemea
 
Hata kama mlitumbuliwa kwa vyeti feki, lakini wehuoni kwamba basi mlipaswa mlipwe stahiki zenu kwa utumishi wenu ulio tukuka kabla hamja tumbuliwa..??
Mkuu hujamuelewa mtoa mada?
Ni kama anawakumbusha walio tumbuliwa kuwa sasa ni zamu yao kumuonyesha Magufuli cha mtema kuni ktk sanduku la kura
 
Ushenzi huo umetoweka pamoja na maelfu ya watu kuumia?
Hakuna vyeti feki maofisini?
Unataka tutoe orodha hapa?
Toa hiyo orodha tuione, tudhibitishe mashaka yako. Otherwise kama uliguswa na sakata lile, ujue kabisa hukustahili mafao.
 
Mimi ni mmoja wa watumishi wa Serikali tuliobainika kuwa na vyeti feki kwenye zoezi la uhakiki wa vyeti feki lililofanyika mwaka 2016.

Nakumbuka takribani watumishi 9000 tulikumbwa na hili sakata la kuwa na vyeti feki. Kwa tathimini iliyofanyika kupitia kundi la sogosi la watumishi tuliokutwa na vyeti feki mwaka 2016 inaonesha kuwa zaidi ya 80% ya watumishi hao waliokutwa na vyeti feki hawana kinyongo na mgombea urais kupitia CCM na wanadai kuwa wangetamani watumishi wenzao waliokutwa na vyeti feki wamuunge mkono mgombea kupitia CCM ili aendelee kuinyoosha nchi iliyokuwa imeoza kwa masuala ya ufisadi, janja janja kwa baadhi ya vigogo waliokuwa wanatumia nafasi zao kuwaingiza ndugu zao serikalini bila kufuata taratibu za Serikali.

Wakaenda mbali kwa kusema na kukiri kuwa in kweli waliwazibia nafasi za ajira serikalini watoto wa maskini waliosoma lakini hawakupata ajira Serikalini kutokana na sababu za baadhi ya wahuni kuziba nafasi.

Kufuatia mjadala unaondelea huko kwenye kundi la sogosi wengi ( majority) wanatoa maoni kuwa watamchagua Magufuli tarehe 28/10/2020 ili aendelee kuinyoosha nchi.

Wengine pia wameomba watumishi ambao wanasema hawajapandishwa madaraja wasiwe na wasi wasi na wamuunge mkono Magufuli kwani tayari ameshaahidi kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara minono kabla kipindi chake kuisha.
Propaganda nyepesi hii... Kwa wale waliotumbuliwa, wao na familia zao, koo zao, rafiki zao, jamaa zao, washirika wao, wapendwa wao, nk.. kazi yao ni moja tuu - kutumbua jiwe tarehe 28/10/2020
 
Back
Top Bottom