Wauaji wakuu wa biashara Tanzania Ni TRA na wapangisha fremu au majengo ya biashara. Serikali iwashughulikie

Mmmmmmm Nani asiyetaka kufanya kazi? Wanafunzi vyuo vikuu maelfu hawana ajira serikalini Wala sekta binafsi unataka wafanye kazi gani? Biashara Bei za fremu ziko juu na TRA wanakalia kooni kwa viwango visivyo rafiki vya Kodi watu wafanye kazi ipi?d
Kuna baadhi ya bidhaa zina kodi kubwa kuliko thamani ya kuinunua!
 
Ukisikia unafiki ndio huu, kila siku mnashangilia mwenyekiti wenu anaposema TRA imevuka lengo la ukusanyaji mapato, unafiki wanakusanya wapi mapato makubwa wakti biashara nyingi zimefungwa? TRA ya AWAMU YA 5 inaharibu biashara kwa kufuata matakwa ya mwenyekiti wa CCM..na bado mpaka muache kuabudu na kusifu kila jambo.
 
Hata yeye keshajua chungu kimekauka bora ahamishie kila kitu Dodoma. Dar haina Doc ya serikali wala Makao Makuu
 
Wewe kichwamaji Tra imeanzishwa na Mkapa ipo hapo siku zote, tatizo siyo Tra bali tatizo ni Magufuli msifungiwe akili zenu kabatini.

Mimi uswahilini nina bar lakini sina interest ya kuiendesha na iko kwenye market nzuri location yake, wakati wa JK kuna mchaga bar yangu ilikuwa inamnyima raha akaitaka kupangisha nikampa akalipa cash kodi ya mwaka na hakuifunguwa hata siku moja lengo lake lilikuwa ni kuiuwa na alifanikiwa, je leo ana jeuri hiyo? Hakuna. Kodi za nyumba tumeanza kupokea za mwezi mwezi hakuna tena cha kodi ya miezi 6/wala miezi mitatu, watu wamepigika na hata nyinyi wenye fungus za ubongo mlizoea kipindi cha kampeni mtakula hela za wagombea safari hii hola hamjaambulia mihondomoro ndio sababu mmeanza kuweweseka.
 
Leo unapinga juhudi za awamu kwenye makusanyo?
 
Baada ya Hali ya biashara kushuka Kodi ya kupangisha ulimshushia huyo mchaga au yeyote aliyetaka kupanga au uliendelea kukomaa kwa Bei ile ile ya wakati mzuri ukijitia hushuki?
 
Watoza ushuru je,frem zimeshuka bei hazina wapangaji
Fremu hazijashuka Bei uliza vinyozi na akina mama wa saloon wakwambie .Wenye nyumba wanakomaa tuuu kodi hawashuki.milango mingi.ya saloon na ya vinyozi wameirudisha sababu Kodi sio rafiki kwa vinyozi na akina mama wa saluni
 
Fremu hazijashuka uliza vinyozi na akina mama wa saloon wakwambie .Wenye nyumba wanakomaa tuuu kodi hawashuki.milango mingi.ya saloon na ya vinyozi wameirudisha sababu Kodi sio rafiki kwa vinyozi na akina mama wa saluni
Iweje awamu hii tu zingine ziligombewa
 
Na bado tutaongea tu lugha moja
TRA na Wenye fremu za maduka wanaongea lugha moja ya kumkomoa mfanyabishara lakini mwisho wa siku TRA na Wenye fremu watajikuta wote wako Hali mbaya sababu mwenye fremu ya kupangisha atakosa wapangaji na TRA watakosa Kodi kote kwa mwenye fremu na mtanyabiadhara mpangaji wa fremu aliyeacha kupanga sababu ya Kodi kubwa ya kupangisha
 
Mishahara ya wafanyakazi inategemea Kodi za wafanyabiashara ndio maana hampandishwi mishahara wala vyeo.Sekta binafsi isipofanya vizuri Kuna siku mishahara yenu itashushwa na mtapunguzwa kazini wewe kenua meno tu
Wewe buku saba aka lumumba siku moja moja dish linashika chanel
 
Siku hazifanani
Hebu tuweke siasa pembeni.....
Wewe ulikuwa una shauri nini kifanyike
Maana kwenye upande wa frame wnaomiliki ni watu binafsi hapo serikali kuwaingilia itakuwa ngumu......Kama ilivyo kwenye kodi za kupangisha nyumba

Ova
 
Lipa kodi mkuu acha kulialika mbona sisi wafanyakazi tunakipa juu kwa juu na tumetulia ,usiwe na akili za wahaini chadema
Mmeanzana nyie kwa nyie, mliambiwa akitumaliza sisi atakuja kwenu hamkusikia sasa yanawakuta, unawasingizia tra hivi humjui anayetuma tena anawawekea na viwango vya kukusanya, ccm oyeeee.
 
Mkiambiwa muwe mnaelewa mnatumia akili sio kung'ang'ania ushabiki wa kijani kibichi, unaona sasa faida ya kumsukumiza mtu mjengoni chama chako kilichofanya? Ambaye hana hata roho ya uwezo wa kiti alichokalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…