Sasa mbona huyo Mungu anataka watu watende mema tu, wakati anajua kuna free will ya kutenda mabaya?
Kwa nini sasa Mungu huyo hapendi maovu?
Kwa nini Mungu huyo hapendi kuona watu wakifanya maovu?
Kama Mungu alijua hapendi na hataki maovu yatendeke, kwa nini aliruhusu free will ya kuweza kufanya mabaya?
Kwa hiyo huyo Mungu alidhamiria kabisa mabaya yawepo ili yafanyike?
Huyo Mungu ana uwehu na ukichaa kabisa. Huyo Mungu hafai kabisa anastahili KUFURUSHWA huko alipo.
Kama Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu na kila alichoumba kilikuwa chema, Sasa haya maovu yaliletwa na nani?
Kama Mungu aliumba malaika wema tu, Shetani aliwezaje kubadilika na kuwa muovu?
Kama Shetani aliweza kubadilika na kuwa muovu, Huoni uumbaji wa huyo Mungu una kasoro na mapungufu?
Huoni uumbaji wa huyo Mungu hauna ukamilifu ndio maana uovu ukaweza kuingia?
Kama Mungu hachunguziki kwa akili za kibinadamu, Wewe ulitumia akili gani isiyo ya kibinadamu kumchunguza ukajua yupo?
Huyo Mungu akiaminiwa yupo, anafaidika nini?
Huyo Mungu asipoaminiwa yupo, anapungukiwa nini?
Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?