Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Wauguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wamepatiwa mafunzo maalum yanayolenga kuwajengea uwezo wa kutambua, kuepukana na kudhibiti msongo wa mawazo unaotokana na mazingira yao ya kazi pamoja na changamoto za kijamii wanazokutana nazo majumbani.
Mafunzo hayo yamenyika leo Jumatano Februari 4, 2026 katika Taasisi ya MOI huku yakilenga kuboresha afya ya akili kwa wauguzi hao, hasa ikizingatiwa mazingira ya kazi yao yanayohusisha kuwahudumia wagonjwa wenye changamoto kubwa za kiafya, hali inayoweza kuathiri ustawi wao wa kisaikolojia endapo haitadhibitiwa mapema
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi MOI, Bi. Stella Kihombo amesema taasisi hiyo imedhamiria kulinda afya ya akili ya watumishi wake ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
“Msongo wa mawazo ukiachwa bila kudhibitiwa unaweza kuathiri utendaji kazi wa muuguzi na kushusha ubora wa huduma kwa mgonjwa, ndiyo maana MOI tumeona ni muhimu kuwapatia mafunzo haya,” amesema Bi. Stella na kuongeza kuwa
“Jifunzeni kutambua dalili za awali za msongo wa mawazo, msibebe mizigo ya kihisia peke yenu, zungumzeni na wenzenu au wataalamu, kwa sababu afya yenu ya akili ni msingi wa huduma mnazotoa,”
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa MOI wa kuboresha mazingira ya kazi na kuhakikisha watumishi wanakuwa na ustawi wa kimwili na kiakili.