Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daahh...poleni sanaa...Mimi nimeshuhudia Amana mtu akizaa chooni kabisaa miaka Ile na nesi anaitwa anajibu hakuna nesi wa chooni ukimaliza kuzaa uje huku tukuhudumie,haya mwingine akizaa pale chini akasaidiwa na wajawazito wenzio ndo wakaja...manesi wa bongo kichomiWalimwambia tu samahani,mtoto ametushinda.....yeye ni C-section....alipojisikia uchungu akakimbilia hospital njian alijisikia kupush,lakini Mwenyezi Mungu alimfikisha hospital salama,wauuguz wakampokea ingali anaendelea kupiga kelele kuwa anataka kupush,kumwingiza leba nesi mmoja akasema huyu ni C-section akapasuliwe nadhani baada ya kuona ule mshono....wakaleta kitanda chao apelekwe chumba husika ...kile kitendo cha kunyanyua mguu apande mtoto akazaliwa na kudondoka chini kwa kuangukia kichwa(mwisho wa siku wakaishia kusema sema "samahani mtoto ametushinda).....ukitaka kisa kingine nikuhadithie nilichoshuhudia mtoto wa kilo 5 alivyokufa mbele ya macho yangu kwa uzembe wa manesi wakati nikijisubiria leba(usiwe mkali tu,kila sekta haikosi watu wazembe ndugu)
Hakuna tume na hakuna wa kufukuzwa hakuna watu wanaolindana kama kada ya afya na hivi wanaaminika ndo usisemeHospitali ni ya wilaya, nesi anayetuhumiwa kufanya uzembe ni wa hospitali ya wilaya, anayeunda tume ni mganga mkuu wa hospitali ya wilaya....!!! Yaani mtuhumiwa anaunda tume kujichunguza..!! Halafu kabisaa tunangoja majibu ambayo yakiwa mabaya yanaweza yakala kichwa cha muunda tume..!!! AJABU NA KWELI
Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.
Happiness, aliyejifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro alisema Oktoba 31 mwaka huu alipohisi dalili za uchungu alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alipofika alipokewa na wauguzi.
Hata hivyo, alisema alipopata uchungu hakupewa ushirikiano badala yake alijifungulia sakafuni.
Juzi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Itikija Msuya alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo akisema ameunda kamati ya kuchunguza ili kubaini kilichotokea siku hiyo.
“Kwa taarifa nilizopewa mtoto alizaliwa zero beating (akiwa amekufa) japo kuna dalili za uzembe ulifanywa na watoa huduma. Nimeunda kamati kuchunguza na watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Dk Msuya.
Akizungumzia hali ilivyokuwa, Happiness alisema baada ya kupokewa hospitalini hapo alifanyiwa vipimo vyote ikiwamo ultra sound na kuambiwa itabidi alazwe asubiri wiki moja iishe kama hatojifungua kawaida, basi atafanyiwa upasuaji.
Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.
Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake. Yule (muuguzi) niliyeenda naye akaniambia nifanye mazoezi ya kutembea, nikawa nafanya hivyo, baadaye hali ikabadilika damu zikawa zinatoka mabongebonge huku nikiwa na uchungu mkali.”
Alisema alipoona hali hiyo alikwenda chumba cha kujifungulia na kumwambia muuguzi aliyekuwepo kuwa anasikia kusukuma mtoto na anatokwa damu nyingi. “Yule muuguzi alinijibu umeweka pamba usije chafua kitanda, nikamwambia ndio nimeweka pamba lakini akaniambia niache kusumbua niendelee kutembea.”
Alisema wakati anarudi wodini kwenye kitanda alichokuwa amelala alishindwa kutembea na kumlazimu kukaa chini huku akiomba msaada kwa kuwa alikuwa akisikia dalili zote za mtoto kutoka na damu ziliendelea kumtoka.
“Manesi walikuja wakaanza kuniambia sukuma huku nikiwa chini sakafuni, nilijitahidi lakini nikawa nasikia nguvu zinaniishia, mmoja wa wauguzi akawa anamwambia mwenzake pokea mtoto si unaona kichwa kile pale.
“Mwenzake akamjibu hapana huyu hasukumi napokea nini? Nikiwa nimelala pale chini wao wako kwa pembeni wananiangalia huku wakiniambia sukuma kwa zaidi ya nusu saa nikajitahidi mtoto akatoka akaanguka chini ndipo wakamnyanyua na kuniwekea kifuani huku wakiniambia niheme kwa kuwa mtoto hakulia alivyotoka ila alianguka chini sakafuni.”
“Baada ya dakika tano bado nikiwa chini sakafuni wakaenda kumuita daktari, huku wanaendelea kumkagua yule mtoto baada daktari kuja ndio akawambia wanitoe pale chini ndipo wakaniweka kitandani na kuanza kunifanyia usafi.”
Mwanamke huyo aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wauguzi hao akidai kifo cha mwanaye ni uzembe wa wakunga na angepewa msaada wangeokoa mtoto huyo.
Mwananchi
Hapa kama hakueleweki fungua kesi mahakamani....Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.
Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake.
inafikirisha
Yes inawezekana piaNi evil spiritual au?
Umeongea wazo jadidiNi Tanzania au?🙌 mie nadhan.labor wangeruhusiwa kuingia na waume zao ujinga ujinga ungepungua..maana wangekatwa kelebu za kutosha na waume zao
Wengine hata kuzipata tu hizo mimba ni kudra za mwenyezi Mungu, unaweza mtafuna mtu, manesi wengine wanakuwaga kama mawakalaJinsi mimba zinavyotesa jamani mtu umeteseka miezi 9 eti unampoteza mtoto wako kwa uzembe wa watu eeeh Mungu tusaidie jamani. Manesi baadhi wamekuwa na roho mbaya sana sijui kwanini ingawa wenye roho nzuri wapo.
Kama unajijua unaroho mbaya kwanini usomee sekta ya afya?? Hatua zichukuliwe kina mama wanateseka sana hasa hospitali za serikali
Sent using Jamii Forums mobile app
Wangefanya kazi yao vizuri hata Mama mwenyewe asingekuwa na shaka nao, lakini kama wamefanya hayo hata kama ungekuwa wewe!Japo kuna uwezekano mtoto alikuwa kafa kabla hajazaliwa
Sure aisee,baadhi yao ni kama wametumwa kuangamizaDaahh...poleni sanaa...Mimi nimeshuhudia Amana mtu akizaa chooni kabisaa miaka Ile na nesi anaitwa anajibu hakuna nesi wa chooni ukimaliza kuzaa uje huku tukuhudumie,haya mwingine akizaa pale chini akasaidiwa na wajawazito wenzio ndo wakaja...manesi wa bongo kichomi
Mimi nashukuru nikifika Cha kwanza mkono natanguliza fastaa na sichelewi leba nkifika nimezaa ndo napata treatment za kistaf balaa... maana najua Mimi ndo ntapoteza kiumbe mwisho wa siku wao hawajali hata chembe,manesi wengi ni wakala wa shetani

Mbaya sanaBad experience. Dah pole na pole kwa huyo mama jamani inauma sana kukosa mtoto wakati angezaliwa vzr tuu
Ukifanikiwa kuzaa mtoto salama na mzima wa afya mshukuru sana Mungu.Duuh [emoji24][emoji24]so many complications
Uishi Maisha marefu madamHaya mambo yapo sana kwenye vituo vya KUTOLEA huduma vya SERIKALI.. Sijui BAADHI YA WATUMISHI WA UMMAH NANI AMEWALOGA .... Ukienda kujifungua private watafanya maandalizi yote LAKINI serikalini utakuta mtu unamwambia nakaribia kusukuma LAKINI YEYE ATAKOMAA BADO AKIREJEA MUDA WAKE ALIOUKADIRIA!!!!! MBAYA ZAIDI UNAKUTA HAMA HATA CHA MAANA ANACHOKIFANYA NA WAKATI MWINGINE UNAKUTA YUKO BUSY NA SIMU..
sasa mziki unakuja mtu anataka kusukuma kweli MARA WATAANZA KUITANA NAOMBA MKASI, NAOMBA KIBANIO CHA KITOVU CHA MTOTO, MARA NAOMBA KADHAA N.K.
. Unajiuliza mtu amefika muds mrefu anakwambia anajisikia vibaya kwanini usimuhudumie???
Tanzania ina wasomi wa kutosha kwa sasa ifike wakati watu ambao hawako tayari kuwahudumia WATANZANIA watafute sehemu nyingine ya kupatia UGALI!!!! Mbona private hukuti hayo manyangamanyanga???
Dawa ni kufukuza kuanzia Mgdanga mfawidhi, katibu wa Afya, Matron, section incharge na wahusika wote!!!!!
Rudisha mtaani na kuleta watu wapya!!!
WATUMISHI wetu wa ummah wanaamini ukiipata kazi ya serikali BASI WEWE NI MFANYAKAZI WA MILELE!!!
Ndiyo maana unakutana na WATUMISHI walevi na tena we anakuwa wamelewa wakati wa KAZI na bado hakuna hatua stahiki zinachukuliwa!!!!!
Kwa utumishi huu productivity na efficiency ni ndogo sana!!! Ifike wakati huu mfumo ufanyiwe upholstery....
Leo Mashirika yetu ya UMMA kama TBA, TEMESA, WAKALA WA MELI, NDEGE n.k yanaendeshwa huku productive na efficiency zikiwa chini mno ni kwa sababu ya MFUMO MBAYA WA UTUMISHI WA UMMAH...
Watu wanapanda madaraja KWA MUDA WALIOTUMIKIA NA SIYO UFANISI, UTEUZI WA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU UNAANGALIA UNAZI KWENYE CHAMA KWA KIWANGO KIKUBWA NA SIYO KUTANGULIZA UTENDAJI, Je katika mazingira HAYA TUTEGEMEE NINI?
Hapo mganga Mfawidhi atawafunika watumishi wake na STORY INAISHIA HAPO....
Mishahara iwe based on performance au kazi zote ziwe za MIKATABA renewable based on performance UONE KAMA KUNA MTU ATAZEMBEA!!!!
Serikali inafanya KAZI NZURI SANA YA KUJENGA MIUNDOMBINU NA KUAJIRI LAKINI WANAOAJIRIWA WAKISHATHIBITISHWA KAZINI BASI WANAANZA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA....
SO SAD.......
Mpaka unajiuliza na haya nayo yanamsubiria RAIS ATOE MATAMKO??????
Context hapa ni uzembe wa manesi katika kumhudumia mgonjwa.Japo kuna uwezekano mtoto alikuwa kafa kabla hajazaliwa
Waziri ataingilia ikiwa tu panampunga mwingi au kuna mtu amelengwa kukatwa kichwaHivi habari kama hii Mtu kama Rais au Waziri Mkuu hawaioni, au ni habari ndogo sana kwao?
Hawajui Manesi kama hawa wamesababisha vifo vya watoto wangapi!?
Kwa habari kama hii ndo nnapomkumbuka Magufuri, japo sikuwahi kukubaliana nae kwa baadhi ya mambo lakini ikija habari ya mwananchi Masikini kunyanyasika, alikubari kusemwa kuwa hafati utawala wa sheria.
hata kama sikuwepo eneo la tukio na simjui huyu dada na ao wauguzi ila nasema hivi " HUYO DADA NDO MSEMA KWELI NA IKO KITU KAFANYIWA KWELI"Hai. Mkazi wa Wilaya ya Hai, Happiness Massawe (39), amegoma kuchukua mwili wa kichanga hospitalini kwa wiki moja akidai kifo cha mtoto wake kimetokana na uzembe wa baadhi ya wauguzi.
Happiness, aliyejifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro alisema Oktoba 31 mwaka huu alipohisi dalili za uchungu alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua na alipofika alipokewa na wauguzi.
Hata hivyo, alisema alipopata uchungu hakupewa ushirikiano badala yake alijifungulia sakafuni.
Juzi, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Itikija Msuya alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo akisema ameunda kamati ya kuchunguza ili kubaini kilichotokea siku hiyo.
“Kwa taarifa nilizopewa mtoto alizaliwa zero beating (akiwa amekufa) japo kuna dalili za uzembe ulifanywa na watoa huduma. Nimeunda kamati kuchunguza na watakaobainika hatua za kisheria zitachukuliwa,” alisema Dk Msuya.
Akizungumzia hali ilivyokuwa, Happiness alisema baada ya kupokewa hospitalini hapo alifanyiwa vipimo vyote ikiwamo ultra sound na kuambiwa itabidi alazwe asubiri wiki moja iishe kama hatojifungua kawaida, basi atafanyiwa upasuaji.
Hata hivyo, alisema Novemba 2 mwaka huu hali ilipobadilika alitoa taarifa kwa muuguzi aliyekuwa zamu, alimpima na kumjibu hasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumpeleka kwenye chumba cha ultra sound tena.
“Tulipofika huko yule muuguzi alimwambia mwenzake nisaidie kumpima huyu mama kwa kuwa sisikii mapigo ya mtoto na ana dalili za kujifungua. Akamjibu mnasumbua; huyu jana si alikuja hapa na nilimpima,” alisimulia Happiness.
Alidai muuguzi aliyempeleka akamwambia, “wewe mpime nataka uhakika, ndio yule muuguzi akanipima huku akisema mnasumbua. Akamuita (muuguzi) njoo usikilize si mtoto anacheza na unasikia mapigo yake. Yule (muuguzi) niliyeenda naye akaniambia nifanye mazoezi ya kutembea, nikawa nafanya hivyo, baadaye hali ikabadilika damu zikawa zinatoka mabongebonge huku nikiwa na uchungu mkali.”
Alisema alipoona hali hiyo alikwenda chumba cha kujifungulia na kumwambia muuguzi aliyekuwepo kuwa anasikia kusukuma mtoto na anatokwa damu nyingi. “Yule muuguzi alinijibu umeweka pamba usije chafua kitanda, nikamwambia ndio nimeweka pamba lakini akaniambia niache kusumbua niendelee kutembea.”
Alisema wakati anarudi wodini kwenye kitanda alichokuwa amelala alishindwa kutembea na kumlazimu kukaa chini huku akiomba msaada kwa kuwa alikuwa akisikia dalili zote za mtoto kutoka na damu ziliendelea kumtoka.
“Manesi walikuja wakaanza kuniambia sukuma huku nikiwa chini sakafuni, nilijitahidi lakini nikawa nasikia nguvu zinaniishia, mmoja wa wauguzi akawa anamwambia mwenzake pokea mtoto si unaona kichwa kile pale.
“Mwenzake akamjibu hapana huyu hasukumi napokea nini? Nikiwa nimelala pale chini wao wako kwa pembeni wananiangalia huku wakiniambia sukuma kwa zaidi ya nusu saa nikajitahidi mtoto akatoka akaanguka chini ndipo wakamnyanyua na kuniwekea kifuani huku wakiniambia niheme kwa kuwa mtoto hakulia alivyotoka ila alianguka chini sakafuni.”
“Baada ya dakika tano bado nikiwa chini sakafuni wakaenda kumuita daktari, huku wanaendelea kumkagua yule mtoto baada daktari kuja ndio akawambia wanitoe pale chini ndipo wakaniweka kitandani na kuanza kunifanyia usafi.”
Mwanamke huyo aliiomba Serikali kuwachukulia hatua wauguzi hao akidai kifo cha mwanaye ni uzembe wa wakunga na angepewa msaada wangeokoa mtoto huyo.
Mwananchi
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏Uishi Maisha marefu madam