Wauguzi walimwambia anawasumbua akajifungua sakafuni, kichanga chafariki

Hizi ndio kada za wito.
R.I.P mtoto.
 
Daahh...poleni sanaa...Mimi nimeshuhudia Amana mtu akizaa chooni kabisaa miaka Ile na nesi anaitwa anajibu hakuna nesi wa chooni ukimaliza kuzaa uje huku tukuhudumie,haya mwingine akizaa pale chini akasaidiwa na wajawazito wenzio ndo wakaja...manesi wa bongo kichomi
Mimi nashukuru nikifika Cha kwanza mkono natanguliza fastaa na sichelewi leba nkifika nimezaa ndo napata treatment za kistaf balaa... maana najua Mimi ndo ntapoteza kiumbe mwisho wa siku wao hawajali hata chembe,manesi wengi ni wakala wa shetani
 
Hakuna tume na hakuna wa kufukuzwa hakuna watu wanaolindana kama kada ya afya na hivi wanaaminika ndo usiseme
 
Haya mambo yapo sana kwenye vituo vya KUTOLEA huduma vya SERIKALI.. Sijui BAADHI YA WATUMISHI WA UMMAH NANI AMEWALOGA .... Ukienda kujifungua private watafanya maandalizi yote LAKINI serikalini utakuta mtu unamwambia nakaribia kusukuma LAKINI YEYE ATAKOMAA BADO AKIREJEA MUDA WAKE ALIOUKADIRIA!!!!! MBAYA ZAIDI UNAKUTA HAMA HATA CHA MAANA ANACHOKIFANYA NA WAKATI MWINGINE UNAKUTA YUKO BUSY NA SIMU..


sasa mziki unakuja mtu anataka kusukuma kweli MARA WATAANZA KUITANA NAOMBA MKASI, NAOMBA KIBANIO CHA KITOVU CHA MTOTO, MARA NAOMBA KADHAA N.K.
. Unajiuliza mtu amefika muds mrefu anakwambia anajisikia vibaya kwanini usimuhudumie???

Tanzania ina wasomi wa kutosha kwa sasa ifike wakati watu ambao hawako tayari kuwahudumia WATANZANIA watafute sehemu nyingine ya kupatia UGALI!!!! Mbona private hukuti hayo manyangamanyanga???

Dawa ni kufukuza kuanzia Mgdanga mfawidhi, katibu wa Afya, Matron, section incharge na wahusika wote!!!!!

Rudisha mtaani na kuleta watu wapya!!!

WATUMISHI wetu wa ummah wanaamini ukiipata kazi ya serikali BASI WEWE NI MFANYAKAZI WA MILELE!!!

Ndiyo maana unakutana na WATUMISHI walevi na tena we anakuwa wamelewa wakati wa KAZI na bado hakuna hatua stahiki zinachukuliwa!!!!!

Kwa utumishi huu productivity na efficiency ni ndogo sana!!! Ifike wakati huu mfumo ufanyiwe upholstery....

Leo Mashirika yetu ya UMMA kama TBA, TEMESA, WAKALA WA MELI, NDEGE n.k yanaendeshwa huku productive na efficiency zikiwa chini mno ni kwa sababu ya MFUMO MBAYA WA UTUMISHI WA UMMAH...

Watu wanapanda madaraja KWA MUDA WALIOTUMIKIA NA SIYO UFANISI, UTEUZI WA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU UNAANGALIA UNAZI KWENYE CHAMA KWA KIWANGO KIKUBWA NA SIYO KUTANGULIZA UTENDAJI, Je katika mazingira HAYA TUTEGEMEE NINI?

Hapo mganga Mfawidhi atawafunika watumishi wake na STORY INAISHIA HAPO....

Mishahara iwe based on performance au kazi zote ziwe za MIKATABA renewable based on performance UONE KAMA KUNA MTU ATAZEMBEA!!!!

Serikali inafanya KAZI NZURI SANA YA KUJENGA MIUNDOMBINU NA KUAJIRI LAKINI WANAOAJIRIWA WAKISHATHIBITISHWA KAZINI BASI WANAANZA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA....

SO SAD.......

Mpaka unajiuliza na haya nayo yanamsubiria RAIS ATOE MATAMKO??????
 
Hapa kama hakueleweki fungua kesi mahakamani....
 
Ni evil spiritual au?
Yes inawezekana pia
Hawa ni zaidi ya ushetani na wengine ni kuzidiwa labda na mambo wanayoyaona kila siku hapo kama vifo na mateso wanayopitia watu

Kwa kweli ni mambo mengi yanayowapelekea kufanya haya ingawa kuna wengine ni down to earth
Wana tabia nzuri na ukarimu mwingi wa kusaidia watu

Najua nesi mmoja yeye hata akimaliza kazi anapita kusalimia wazee na wagonjwa walioko manyumbani

Ila kuna wauwaji wengi pia wanaojificha kwa mwili wa binadamu
To be honest I don't like hospitals
 
Aloo hii habari imenikumbusha wakati namsindikiza dada angu kwenda kujifungua vile tunafika kujiandikisha tu yule nesi kutuona kasonya (maana mda wake ulikuwa umekwisha anajianda kutoka ) tukajiuliza kama huduma ndo hizi tunanyaliwa na kusonywa namna hii na nesi itakuaje ?tukajipa moyo tukajiandikisha vizuri japo alijua kabisa tumeona alichokifanya..basi akawekwa chumba cha uangalizi kusubiri kuingia leba rum alikaa mle hakuna nesi alifika mpaka chupa ikapasuka akaita nesi bila msaada badae kajitokeza mmoja kaja lkn mtt alikuwa amekaribia kutoka(kichwa kinaonekana )akatembea kwa kujikaza hivo hivo hadi leba rum ilibaki kidogo mtt adondoke sakafuni..hawa manesi baadh yao hawana huruma ndo maana wanastaafu na laana za wazazi..tena kama wanawake manesi baadhi yao wanaroho mbaya mno
 
Wengine hata kuzipata tu hizo mimba ni kudra za mwenyezi Mungu, unaweza mtafuna mtu, manesi wengine wanakuwaga kama mawakala
 
Japo kuna uwezekano mtoto alikuwa kafa kabla hajazaliwa
Wangefanya kazi yao vizuri hata Mama mwenyewe asingekuwa na shaka nao, lakini kama wamefanya hayo hata kama ungekuwa wewe!
 
Sure aisee,baadhi yao ni kama wametumwa kuangamiza
 
Sure aisee,baadhi yao ni kama wametumwa kuangamiza
Bad experience. Dah pole na pole kwa huyo mama jamani inauma sana kukosa mtoto wakati angezaliwa vzr tuu
Mbaya sana
 
Uishi Maisha marefu madam
 
Japo kuna uwezekano mtoto alikuwa kafa kabla hajazaliwa
Context hapa ni uzembe wa manesi katika kumhudumia mgonjwa.

Wangewajibika ipasavyo pasingelikuwa na lawama, maana hayo mengine ni matokeo ya kawaida kwa wajawazito wakati wa kujifungua "labor".
 
Waziri ataingilia ikiwa tu panampunga mwingi au kuna mtu amelengwa kukatwa kichwa
 
hata kama sikuwepo eneo la tukio na simjui huyu dada na ao wauguzi ila nasema hivi " HUYO DADA NDO MSEMA KWELI NA IKO KITU KAFANYIWA KWELI"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…