Waukraine watakiwa wachaji simu zao mapema wakati Berluscon amlaumu Zelensky

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Shirika la umeme la Ukraine ,Ukrenergo limewataka wateja wake wawe wakichaji simu zao mapema na tochi kwani hali ya upatikanaji wa umeme imezidi kuwa mbaya huku hofu ya kushambuliwa zaidi kwa vinu vya umeme kutoka majeshi ya Urusi ikiongezeka.

Katika nasaha zake katika kipindi hiki cha baridi kali shirika hilo limewataka wanachi pia kujiwekea akiba ya maji na kutayarisha soksi maalum za kuzuia joto bila kusahau kukumbatiana kwa ndugu na familia ili kuhifahdhi joto lao lisipotee.

Kwa upande mwengine aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Italia kwa miongo kadhaa na tajiri mkubwa nayemiliki timu za mpira Silvio Berlusconi amenukuliwa kwenye kampeni za kisiasa akimlamunu raisi Zelensky wa Ukraine kwa kumlazimishi raisi Putin wa Urusi kuivamia nchi yake.

 
Huyo Silvio anatumia matatizo ya Uikrane kujipatia kura Kisha hàkuna atakachofanya Cha maana,mgombea wa Iran kwenye kàmpeni zake kipindi Cha nyuma Ahmednejad kama sijakosea aliahidi kuifuta Israel kwenye ramani,kilichovutia mpaka anatoka madarakani hakuifuta.
 
kama ingekuwa Tanzania haina hata haja ya kuwaambia wachaj simu zao watanzania ikifika asubuh tu wote zinasoma battery full 100%
 
Kwani wao wanashindwa kuishambulia vinu vya kifua umeme vya Russia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…