Waumini wa FGBF wampa zawadi ya nyumba Askofu Kakobe na Mkewe

Angesema amejenga mwenyewe, watu na serikali wangehoji ametoa pesa wapi? amelipa kodi? Anafanya biashara gani?
Sasa kucheza na mind, imebidi kutengeneza mchezo wa kusema amejengewa na waumini wake (tena sio waumini wa Dar!), kwa muda wa miaka 12 nk.

Hizi dini ni usanii sana.
 
Kwenye picha ya nyumba ya Askofu Bagonza atuwekee hapa!
 
Acheni wivu wakuu !
 
Hilo jumba ni next level. Ile exterior ni balaa. Ukuta tu nadhan unapata kibanda uswahilini.

Kubwa mno hilo jumba
Yeah,ndani vyoo na mabomba ni dhahabu tupu,,talazo imetoka europe na america,
Malumalu zile za kisasa kabisa kama zile alizozikuta Adili kwenye mji wa ajabu,,
Kila kitu kiko automated,kuanzia geti hadi toilet,,
Kuna ATM za maziwa,nyama choma,mvinyo wa italy,birian,vyuku etc,
Kitanda ni platinum,magodoro ya sufi,mapazia ya hariri,
Tv ya nchi 100,yenye chanels 2000,
Ni pazuri mno kwa kweli.
 
Huyu Mzee bila Zengwe Kazi yake imeonekana.

Ameweza fundisha Imani ya kumjua Christo watu wote tofauti walio na Elimu ya Juu kuanzia ma Prof mpaka wale wachini wasio na Elimu.

Sasa unakuta mtu Hana maisha wala mbele hajui lakini ata diss
 
Kwa Kuongezea hapo kwenye upigaji,na mengineyo!

1.Ameanzisha kanisa mwaka 1989 akiwa na waumini 13

2.Ana makanisa zaidi ya 1000 Tanzania yote

3.Sadaka huwa haikatwi kodi

4.Ana kanisa na waumini zaidi ya 5000 nchini Korea kusini na yeye ni maarufu mno

5.hakuna mchungaji yoyote wa kiroho,labda umtoe Moses Kulola (Marehemu) anayeheshimika na waumini kama Kakobe,na kupendwa nao

6.TRA walimkuta na sh Bilioni nane cash Bank zenye maelezo yaliyonyooka, ikabidi TRA wamchunguze mke,watoto, au ndugu zake kwa kushirikiana na TISS kama wana biashara ingine

7.kuna Kitu Kinaitwa Imani, Ukiacha TAG ya moses Kulola hakuna kanisa lingine la kiroho linamkuta Kakobe kwa waumini Tanzania...na hawa waumini wanayoa sadaka,na sadaka zinagawanywa kati ya wachungaji, na familia ya kakobe...


Hitimisho: Angeamua Kuishi kama wachungaji wengine wanavyoishi, nigeria,us au uk wale wachungaji wa kinegiria au kina bushiri ningepata mashaka nae..
ila kama unajitambua...ukimuangalia KAKOBE na hawa wachungaji wengine wa Kiroho unamuona kabisa yeye ni wa tofauti kabisa....

Ukiambiwa KAKOBE umlinganishe na hawa wachungaji wengine wa kiroho utamlinganisha na nani? mimi Labda Moses Kulola...na Mwakasege (japokua mwakasege ni mwalimu)

Niambieni usanii wake ni upi? alishazalisha mke wa mtu,alishaua watu? alishatembea na waumini zake? alishavaa pete za ajabu? alishalewa hadharani?

Naomba nisamehewe kama nimekwaza watu ni mawazo yangu tu! na mm ni mkatoliki saafi!

Ahsanteni
 
wamefanya vyema, wampe tu!
 
Una roho ya ki-maskini na hujui wokovu.

MUNGU ana kila kitu ila alipewa sadaka na Habili na kaini.

Mungu ameumba vitu vyote, fedha na dhahabu ni vyake lakini bado tunamtolea.

Elewa, zawadi na sadaka ni appreciation na si kumpa mtu kwakuwa hana.

Mungu ameagiza kutoa, na hapo ndipo ananpopimwa mwanadamu uaminifu wake , "Anania na Safira walidanganya kuhusu kiwanja walichouza na Walikufa" Mungu aliwapima uaminifu na si kwamba alitaka fedha toka kwa anania na Safira.
 
'Niambieni usanii wake ni upi? alishazalisha mke wa mtu,alishaua watu? alishatembea na waumini zake? alishavaa pete za ajabu? alishalewa hadharani?'

Huyu jamaa alikua anawaambia waumini wake wakiingia kanisani kwake na vitu vya dhahabu kama Pete,Mikufu,heleni wanamkabidhi avichome mote maana ni vitu vya shetani hivyo.

Siku anahojiwa na Pasco Mayalla akaombwa aonyeshe wapi hua anachomea hivyo dhahabu za waumini wake,aling'aka hatari saaana.
 
"6.TRA walimkuta na sh Bilioni nane cash Bank zenye maelezo yaliyonyooka, ikabidi TRA wamchunguze mke,watoto, au ndugu zake kwa kushirikiana na TISS kama wana biashara ingine'.

Hii sio kweli,zile pesa zilitaka kupigwa pini na ndio chanzo cha Kakobe kuunga mkono juhudi haraka sana,since then mpk leo hafurukuti tena.
 
Umeongeza munyu mkuu !
 
Una roho ya ki-maskini na hujui wokovu.

MUNGU ana kila kitu ila alipewa sadaka na Habili na kaini.

Mungu ameumba vitu vyote, fedha na dhahabu ni vyake lakini bado tunamtolea.

Elewa, zawadi na sadaka ni appreciation na si kumpa mtu kwa

LIBARIKIWE TUMBO LILILOKUZAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…