Waumini wa FGBF wampa zawadi ya nyumba Askofu Kakobe na Mkewe

Askofu Alex Malasusa amestaafu anaishi kwa shida?
Au tupe mfano wa Askofu anayeishi kwa shida
 
Ile kesi ya mabilioni aliyoshitakiwa na wachungaji wake iliisheje ile
Jaji aliwauliza kama kweli wana nia ya kuendelea na kesi sababu ukiisoma katiba ya FGBF utaona Kakobe ndio FGBF na FGBF ndio Kakobe, sasa unaweza vipi kumhoji mtu kutumia 'vibaya' fedha yake mwenyewe?? Jamaa wakajitafakari na kuamua kufuta kesi
 
Huyu mzee ana historia yoyote na Marehemu Askofu Moses Kulola?
Askofu Zakaria Kakobe ana historia ya askofu Kulola.

Kumbuka Moses Kulola ndiye baba wa kiroho wa Kakobe. Kakobe emekulia kwenye kanisa la Kulola pale Temeke wakati anaanza safari yake ya wokovu...
 
Sadaka na michango yote si anachukuaga yeye au?
 
Askofu Zakaria Kakobe ana historia ya askofu Kulola.

Kumbuka Moses Kulola ndiye baba wa kiroho wa Kakobe. Kakobe emekulia kwenye kanisa la Kulola pale Temeke wakati anaanza safari yake ya wokovu...
Oooh sikulijua hili.
 
TeAskofu Zakaria Kakobe ana historia ya askofu Kulola.

Kumbuka Moses Kulola ndiye baba wa kiroho wa Kakobe. Kakobe emekulia kwenye kanisa la Kulola pale Temeke wakati anaanza safari yake ya wokovu...
Tena Askofu Kakobe na mkewe Pastor Hellen walikuwa wanamtegemeza Askofu Moses Kulola kwa miaka wakiwa EAGT; na hata sasa bado anaendelea kutegemeza huduma mbalimbali za ndani na nje ya TANZANIA kwa mali na fedha nyingi ! Ushahidi upo.
 
Abarikiwe sana huyu mzee
Tena Mungu ampe maisha marefu na afya tele Askofu Kakobe akazidi kuwa baraka kwa mataifa mengi.
Na alaaniwe atayemlaani askofu kakobe. Sema Amen !
 

Attachments

  • FB_IMG_1606448809998.jpg
    26.1 KB · Views: 26
Asante ! Ni kweli anastahili kupewa heshima kwa kuwa kielelezo kwa watumishi wa Mungu kutokana na tabia na utumishi anaotenda hata sasa kwa karibu miaka 40
 
Asante ! Ni kweli anastahili kupewa heshima kwa kuwa kielelezo kwa watumishi wa Mungu kutokana na tabia na utumishi anaotenda hata sasa kwa karibu miaka 40
Hakika. Pia kuna jambo moja ambalo ninaliona linaweza kuboreshwa pale kanisani kwake.

Yesu alikuwa karibu na wenye dhambi hakuwabagua. Alikaa nao karibu mpaka mafarisayo wakalalamika....

Asikibali kanisa kugeuka kuwa la kifarisayo.

Nimeongea kwa lugha ya ndani sana
 
Tena Askofu Kakobe na mkewe Pastor Hellen walikuwa wanamtegemeza Askofu Moses Kulola kwa miaka wakiwa EAGT; na hata sasa bado anaendelea kutegemeza huduma mbalimbali za ndani na nje ya TANZANIA kwa mali na fedha nyingi ! Ushahidi upo.
Anachokifanya Kakobe leo ni maono aliyoyapata na kuyaweka kwenye kipeperushi cha UAMUZI NI WAKO... enzi alipokuwa mkurugenzi wa G.E.T.

Aliweka roadmap namna injili atakayosimama nayo. Injili isiyochujwa na yenye kutumia nyanja zote za kiteknolojia kuufikia Ulimwengu

Alisema sasa ni wakati wa Afrika kuihubiri Injili ya kweli kwa ulimwengu.

Kakobe siyo wa mchezo mchezo na hatafuti ukubwa...
 
Hapo kwenye kuikosoa serikali kuna kasoro kubwa sana. Kakobe ni mnafiki sana, akibanwa na serikali anarudi kuipigia magoti na kuilamba viatu.
Angalia hichi anachokifanya sasa, ni kumsifia Magufuli tu.

Suala la imani yake mimi sijui, lakini suala la kupigania haki, Kakobe ni MUOGA, MNAFIKI na TAPELI.
 
Waumini kwa hiari yao baada ya kutafakari nyumba aliyojenga miaka mingi kabla kuanza utumishi wake; haina hadhi ndipo wakapata wazo la kutoa changizo ya kumjengea jumba lenye hadhi ya kimataifa kwa utukufu wa Mungu anayemtumikia askofu Kakobe.
Mkuu acha maneno mengi ya kusifia tu, weka picha ya hilo hekalu alilojengewa Askofu Kakobe, weka na gharama zilizotumika kulijenga.

Mtumishi Kakobe anakula vinono huku kondoo wakiteseka kwa njaa kali.
 
Kumsifia mtu pale anapofanya jambo jema siyo vibaya! Kuna wakati wa kukosoa na wakati wa kusifia.
 
Askofu Zakaria Kakobe ana historia ya askofu Kulola.

Kumbuka Moses Kulola ndiye baba wa kiroho wa Kakobe. Kakobe emekulia kwenye kanisa la Kulola pale Temeke wakati anaanza safari yake ya wokovu...
Kwanini Kakobe alijitoa kwa Kulola (EAGT) ili kwenda kuanzisha dhehebu lingine la FGBFC?
Kwanini hakubakia hapo hapo EAGT ili kuendeleza kile kilichoanzishwa na Kulola,
Aliona biashara ya injili inalipa?
Aligombana na Kulolam
Aliona Kulola (EAGT) ni wazushi?
 
Mbona kawaida tu! Hata mitume wa Yesu nyakati za Kanisa la kwanza waliachana kwa nia ya kueneza Injili ya Kristo.Kwa hiyo haikuwa ajabu Kakobe kumwacha Kulola lakini pamoja na hayo Kulola alikuja kuikubali na kuibariki huduma ya Kakobe! Na hadi mzee Kulola anafariki ameondoka akiitambua huduma ya Ask.Kakobe kuwa ni huduma ya kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…