Waumini wa KKKT Kijitonyama waanza kuulizwa namba za Bahasha za Sadaka mlangoni

Waumini wa KKKT Kijitonyama waanza kuulizwa namba za Bahasha za Sadaka mlangoni

Dah! Hii nchi inaelekea pabaya. Maana kwa sasa faraja ya wananchi, ipo kwa hao wachungaji, Mitume na Manabii! Na wengine ni bar na kubet!

Na siyo tena kwa viongozi wenye dhamana nchini.
Nchi haiwezi kwenda vibaya, wananchi ndiyo watakaoenda vibaya kwa kushindwa kutumia akili kwa maana reasoning na roho kwa maana ya intuition.
 
Nauliza tu, kwani Eliona Kimaro ni Yesu ?, Kama so Yesu mbona waumini wanaangaika ?
 
Hakuna maamuzi yatakayotenguliwa amepigwa likizo ndo imetoka hyo , akirud atapangiwa karagwe huko...!!
Hawezi kupangiwa Karagwe kwakuwa yeye ni Mchungaji wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani tu.
 
zote ni biashara zilezile tu.Ali bakari na bakari Ali
Ndio maana siwezi kuhama RC. Maparoko huwa wanahamishwa na hakuna anayeuliza , kanisa letu linaongozwa na Utii tu
 
Sasa hizo ibada za Morning glory mbona wanaingia hata wasio wakristo? Hao Viongozi kulikon? Au ndo wamechanganyikiwa?
Mtu yeyote anaruhusiwa kuingia kanisani au msikitini bora yuko sawa tu. Mpagani, freemason, Sho*a, asiyejua kusoma wala kuandika, professor nk

Wengine tushasali kanisani, msikitini, temple na ghetto kikubwa Mungu hana ubaguzi na kanisa au msikiti sio private property
 
Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama Dk Eliona Kimaro kupewa likizo, ibada ya asubuhi (Morning glory) imefanyika huku idadi ya waumini ikiwa ndogo tofauti na ilivyozoeleka.

Licha ya uchache huo wa waumini pia baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wamehakikisha ibada hiyo inafanyika kutokana na baadhi ya waumini kuzuia jana ibada ya jioni (evening glory) kufanyika baada ya kuandamana na mabango wakimtaka mchungaji wao Dk Kimaro.

Mapema jana Jumanne asubuhi, Januari 16, 2023 ilisambaa video katika mitandao ikimuonyesha mchungaji huyo akiwaeleza waumini wake kuwa amepewa likizo ya siku 60 baada ya kuitwa katika ofisi ya msaidizi wa askofu na kufanya kikao na mkuu wa Jimbo la Kaskazini.

"Semina yetu ni ya wiki mbili (Semina ya neno la Mungu), lakini niliitwa ofisi ya msaidizi wa askofu, tulikuwa na kikao na Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mchungaji (Jacob) Mwangomola.
Nimepewa barua ya likizo ya siku 60 kesho asubuhi (leo Jumatano) atahubiri Mchungaji Anna na ataendelea kuwa Mchungaji wenu," amenukuliwa kwenye video hiyo.

“Kwa mujibu wa barua nitarudi Machi 17 (2023) na sitakuja hapa, barua inanilekeza kuripoti Makao Makuu ya Dayosisi. Kwa hiyo mimi ni Mchungaji wa Lutherani nina heshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo na maadili…

“Pia kwa neema ya Mungu kwa sababu hiyo imenilazimu kutii na kwenda kwenye hiyo likizo na baadaye kuripoti kwenye ofisi ya askofu kama nilivyoelekezwa,” anasema Mchungaji Kimaro katika video hiyo.

Mbali ya video hiyo, ipo nyingine iliyosambaa ikiwaonyesha baadhi ya waumini wa usharika huo wakiangua vilio, wakati mchungaji huyo akifanya maombi ndani ya kanisa hilo wakati akiaga.

Mwananchi ilifika kanisani hapo leo Jumatano Januari 18, 2023 saa 12:25 asubuhi na kukuta ibada hiyo ikiendelea huku baadhi ya viongozi wakiwa kwenye lango kuu wakitaka kufahamu baadhi ya taarifa za waumini ikiwemo jumuiya anayosali na kama ana namba.

Hata hivyo, mmoja wa waumini ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema, watu wamevunjika moyo kutokana na kilichofanyika haiwezekani mchungaji apewe likizo ya siku 60, wakati ndio mwanzo wa semina.

“Pamoja na kuwepo mgawanyiko kila mtu ana imani yake siyo wote waliokuja kusali hapa wanafurahishwa na kilichotokea, ndio maana hata viongozi wanajitahidi ibada hii isivurugike kama ile ya jioni watu ni wachache,”alisema muumini huyo.

Muumini mwingine Helleni Minja anayefanya biashara nje ya kanisa hilo amesema, asubuhi ni vigumu kuzuia ibada kutokana na watu wengi kwenda kazini lakini ibada ya jioni na Jumapili hazitafanyika hadi mwafaka upatikane.

MWANANCHI
Hii inatoa picha kuwa anatolewa Ili watu waendelee kukusanya pesa, kama hii taarifa basi jibu ni kuwa Kuna kitu alikuwa anakisimamia hakijawapendeza wengine

Kuna muda waumini hujitahidi kujenga ila viongozi hupindisha mirija ya mapato na kuweka kwao ni changamoto kweli kweli ,ndio maana watu wengi wamejitoa katika mas'ala ya dini , lakini msichoke kumuabudu mwenyezi Mungu
 
Ningekuwa Malasusa ningemsweka kijijini ambako hata network haikamati ili aache kurusha vi clip vyake vya kujimwambafy.....
 
Hakuna maamuzi yatakayotenguliwa amepigwa likizo ndo imetoka hyo , akirud atapangiwa karagwe huko...!!
Bagonza yupo Karagwe lakini anasikika nchi nzima kuliko waliopo Azania Front. Kama Mungu ameweka kitu kwa mtu binadamu wanajisumbua sana.
 
Bagonza yupo Karagwe lakini anasikika nchi nzima kuliko waliopo Azania Front. Kama Mungu ameweka kitu kwa mtu binadamu wanajisumbua sana.
Huyo bagonza alipata hipe Kwa Kwa kufokeana na Maghufuli , now kwisha habar yake , Hana Kiki yoyote ya kumuweka mjini .....!! Labda awatukane viongozi wake wa dini
 
Back
Top Bottom