Waumini Wa Mwamposa Moshi Wasema''Alituponya hata kesho akija tunaenda

Waumini Wa Mwamposa Moshi Wasema''Alituponya hata kesho akija tunaenda

Saint Ivuga huo uponyaji ni kama tiba? Hakuna kanuni ya kiroho inayotumika kwenye miujiza? Ni kwa nini hao Manabii wako bize "kuponya" badala ya kuhubiri Injili ya Uponyaji?
kama hawa wana majini utawahubiria nini zaidi ya kuyatiumua majini yao ? Yesu mwenyewe hakumpiga injili mgerasi.Baada ya majini kuondoka yule mgerasi alijitambua mwenyewe
 
Tatizo ni Wanaume wa Kichaga, no responsibilities kwa Wanawake wao, wanawatelekeza Migombani kukimbilia mjini wakati wao (wanawake) ni binadamu pia, wana mahitaji, ndo maana wanatafuta njia mbadala.

Take care of your women!
 
YESU aliponya kwa kutumia hadi mate na matope na watu walimfuata hawakuacha kumfuata sembuse kutumia sabuni

Nalifahamu wengi hutumia habari hii kama kielelezo cha kuwafanyia wengine vituko hapa kuna vitu viwili katika hii habari inayopatikana Yohana 9 kasome chapter yote na si unakuja na kamstari utaelewa dhumuni la muujiza huu na hitimisho alilotoa Yesu mwenyewe na kwanini yule mtu aliponywa upofu kwa mtindo huu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
sidhani kama una jua ila
Wengi wanaoenda huko wana matatizo makubwa na hawana choice na wengine wanapona amini usiamini.

"Ceteris Paribus"

Kuna baadhi ya watu wameshazunguka Hospitali zote na hawajapata tiba.
Hawana kimbilio zaidi ya kuzunguka kwenye wachungaji na manabii .

Na kuna shuguda watu wanapona.
Mimi nimeona kwa macho yangu.

Maombi huponya. Japo hutaweza kuona kila mtu akipona haiwezekani.

Kwa hio msiwabeze watu.

Siku ukipigwa na gonjwa ( japo sikuombei) ndio utajua ninachojaribu kukueleza.
Mimi ningekushauli ukae chini utafakari akiri yako uiulize kuwa ni Nani alikuroga hadi hutaki kujiondoa ndani ya box? Mnatupatia Sana Kazi Ya kuwaelimisha, ngoja nikuambie ingekuwa hao wachungaji wanaponyesha kungekuwa Hakuna watu mahospitalini, naomba nirudie kungekuwa hao watu wanaponyesha kungekuwa Hakuna watu mahospitalini Kama hujaelewa ngoja niendelee kidogo, hivi unajua kuwa kuna watu wana Dawa Ya kumfanya mtu akapita Kwa watu pasipo watu kumuona inhali anapita wazi mchana kweupe? Hivi unajua kuwa kuna watu wanamfanya mtu kuwa ndondocha? Kama uliwahi kusikia basi hivyo hivyo wapo ambao wanaweza kuuzuia ugonjwa wako kwa muda usioonekane Lakini bado unaumwa na utaumwa na utakuja baadae Sana kushangaaa ugonjwa kuuona ukiwa umefika mbali, nikuulize tena hivi unajua maaana ya mazingaombwe? Kama unajua Sina haja kuendelea na hilo nikukumbushe tu kuwa nabiii Mchungaji Yule wa Mwenge aliesema kuwa umeme atauzuia kakobe alipoaanza alisema viwete wanapona, wenye ukimwi wanapona je ulilisikia hilo? Sasa nikuulize Kama ulilisikia hilo wangapi wameishapona? Na wapo wapi? Na Kama wanapona Kwa nini pale jirani yake hospital ya mama Ngoma wamejaaa hao wagonjwa?

Acha kutupa Kazi Ya kukuelimisha kitu kidogo Sana cha uelewa Mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kondoo mkia wake umejaa mafuta tele ila bado analilia mafuta feki ya mchungaji wake.
 
Tuache watu na imani zao hivi mnadhani wangekuwa hawaponywi wangejazana pale kawe kwenye huduma yake?Watu wanatembea kwa umbali mrefu kutafuta usafiri wa kwenda kawe kukanyaga mafuta tu haijalishi ni ya kichawi au kiMungu lkn watu kwa imani zao wanapona.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha na wewe kutupatia Kazi Ya kukuelimisha unatuambia kuwa angekuwa haponyi watu wangeenda huko, mbona unauliza swali la kitoto Sana? Sasa kule Kwa babu wa loliondo hukuona watu? Hukuona msululu toka mikoa mingne? Je aliponyesha? Na Kama aliponyesha Nani alipona? Kwa nini haendelei? Ninapataga Sana uchungu kuona watu wanauliza mambo madogo Sana ambayo watu wangeelewa Kwa kujiuliza tu maswali tu machache, yani uende kuponyesha watu halafu wafe upelekwe na MUNGU kusaidia watu halafu kiwe kilio hapo tena, yani unaenda kuwapelekea unafuuu umetumwa na MUNGU yaende kutokea majanga duuuuh watanzania sijui tulilogwa na Nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume wengi dini hawana.

WANAWAKE WENGI NDIO WANA DINI
Swali sio wenye dini bhana, hivi wewe unamkumbuka kakobe? Unamkumbuka Lakini kakobe enzi za 1996 ?unamkumbuka kakobe watu walivyo kuwa wanajaaa kule Mwenge? Unakumbuka kuwa watu walikuwa wanatoka had morogoro? Unakumbuka kuwa habari ya mujini kipindi hicho ilikuwa ni kakobe? Unajua kuwa Alikuwa akiwaponya hadi watu wenye ukimwi? Viwete wanatembea? Unakumbuka? Leo nenda kwenye kanisa la kakobe baba Hakuna mtu wapo wa kuhesabu tu hiyo ni baada ya watu kugundua kuwa Alikuwa muongo, Hakuna aliekuwa anapona,
Mimi nikuambie kitu Mkuu kanisani ni sehemu ya kwenda kufundishwa Namna Ya kumtumikia MUNGU, kumtumikia MUNGU, Namna Ya kuishi Kwa matendo yanayomfurahisha MUNGU, Namna Ya kufuata zile sheria za amri kumi za MUNGU, kanisani sio sehemu ya kufundishwa Namna Ya kutajirika, sio sehemu ya kufundishwa Namna Ya kumpata mchumba, Namna Ya kumzuia mwenza asitoke nje Namna Ya kupata Kazi Namna Ya kujazwa pesa, sio sehemu ya kufundishwa Namna Ya kupata gari Au nyumba Au Kazi, kanisani ni sehemu takatifu ukifika unapaswa hata kuongea uongee Kwa unyenyekevu Kama unavyowaona wachungaji wa kiroma wanavyoongea Kwa unyenyekefu wa hali ya Juu, kufanikiwa kimaisha na na kupona magonjwa na kuepuka majanga huwa ni matokeo tu Ya Kazi uliyoifanya ya MUNGU kwa kueneza Upendo, kujali watu, kusaidia Watu, kuthamini watu, kuthamini wahitaji kuepuka zile amri kumi ndio mavuno yako unayapata Kwa kufanikiwa hitaji lako, kumbuka kuwa mafanikio unayoyataka ni sawa na mtu anaejituma katika Kazi mwisho hupata Mali kutokana na Kazi aliyoifanya ikazaa mafanikio, hivyo MUNGU alivyosema kuwa asiefanya Kazi na asile alimaaanisha kuwa hata hayo mafanikio unayoyataka ya kupona ugonjwa na kuepuka majanga ni matokeo ya Namna utakavyomtumikia MUNGU kwa kumnyenyekea, kumtumikia Kwa kuwapenda wenzio, kuwasaidia, kuwathamini na kumtumikia MUNGU kwa Jumla hao wanokusanya Watu tu wakatoa Sauti kubwa hukusanya had wauwaji watesaji, wasinzi eti njoo ukanyage mafuta upone MUNGU akuponye, utatoka kuuwa ukakanyaga mafuta ukapona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisani sio sehemu ya kufundishwa Namna Ya kutajirika, Namna Ya kupata gari Au nyumba Au Kazi,
NINI? HUJUI KITU

Petro alikuwa maskini wa kutupwa alivua samaki usiku kucha hakupata kitu akaenda kwa Yesu alivyoona umaskini umemzidi .Yesu akamfundisha namna ya kutajirika chap chap akamwambia nenda katweke kilindini akavua samaki wemngi hadi akaita vyombo vingine vije kumsaidia kubeba utajiri mkuu wa samaki aliopata

Kuna siku walidaiwa kodi na pesa wakawa hawana Yesu akamfundisha petro pesa inapatikanaje chap chap akamwambia Nenda kavue samaki mmoja tu ukimvua mfunue mdomoni utamkuta ana pesa ya kutosha njoo nayo!!!

kanisani sio sehemu tu ya kusoma liturjia wewe!! na kutembea taratibu unanyata kama bibi harusi na kanzu!! BIBLIA inasema utajiri na heshima unapatikana kwake

Mithali. 8:18

Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
 
Siri ya kupona ugonjwa ulioshindikana hospital, Siri ya kuepuka majanga, Siri ya kupata kile unachokihitaji na Siri ya mafanikio, nikumtumikia MUNGU kwa kumkiri MUNGU, kumuishi MUNGU na kufuata maelekezo Yote ya MUNGU pasipo kupindisha hata chembe.
Mtumikie MUNGU kwa kumuona kuwa yeye ndio kila kitu katika maisha yako, fanya Jambo moja zuri kila Siku iendayo Kwa MUNGU Jambo litakalomfurahisha MUNGU mkiri MUNGU na muishi MUNGU kwa nguvu zote na mpenyeze MUNGU aingie ndani mwako kwenye mwili wote mpenyeze kwenye damu na acha kumuumiza binadamu mwenzio, Maende Sana binadam mwenzio kuliko unavyojipenda wewe, wapende watoto Kwa hisia wapende wanawake Kwa hisia hawa ni viumbe dhaifu, wapende Sana na wapende Sana wahitaji, saidia watu shida zao kadri uwezo utakavyoruhusu, mtaje MUNGU kwa kila Jambo ulifanyalo tembea na biblia ukiwa Safari, jaza biblia nyingi nyumbani kwako ikiwezekana kila chumba weka biblia mtangulize MUNGU kwa kila Jambo penye ugumu mkabidhi MUNGU kwa hisia kuwa yeye ndie atatue, usiogope kumtaja MUNGU na mwandike MUNGU kwa herufi kubwa jishushe Kwa wenzako na Yote unayoyafanya Kwa Nia ya kumuomba MUNGU usimuombe MUNGU kwa kuwaonesha watu kuwa wewe unampenda MUNGU mpende MUNGU kwa moyo wako wewe na yeye thamini watu

Ukiyatimiza hayo waweza tembea kifua mbele ukiwa na mawazo ya kujiamini kuwa Hakuna baya litakalo kutokea na maisha yako yatanyooka kila penye ugumu MUNGU wako atatatua tu, watakuja wachawi wakuloge hutalogeka, watakupangia mabaya wabaya wako yatawarudia wao, kila Jambo baya litakuja litamkuta MUNGU yuko mbele yako atapigana nalo

Hao manabiii ni ajira ya kisayansi wamejiajiri ili maisha yaende wanatumia mambo mengi yakutisha Kwa kuwatumia watu wasiomjua MUNGU kufanikisha yao hata huyu mwamposa ataenda mwisho watamkimbia atakuja mwingne tena mtahamia kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NINI? HUJUI KITU

Petro alikuwa maskini wa kutupwa alivua samaki usiku kucha hakupata kitu akaenda kwa Yesu alivyoona umaskini umemzidi .Yesu akamfundisha namna ya kutajirika chap chap akamwambia nenda katweke kilindini akavua samaki wemngi hadi akaita vyombo vingine vije kumsaidia kubeba utajiri mkuu wa samaki aliopata

Kuna siku walidaiwa kodi na pesa wakawa hawana Yesu akamfundisha petro pesa inapatikanaje chap chap akamwambia Nenda kavue samaki mmoja tu ukimvua mfunue mdomoni utamkuta ana pesa ya kutosha njoo nayo!!!

kanisani sio sehemu tu ya kusoma liturjia wewe!! na kutembea taratibu unanyata kama bibi harusi na kanzu!! BIBLIA inasema utajiri na heshima unapatikana kwake

Mithali. 8:18

Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
Hayo ndio wanayotumia kuwadanganya wasio jua Kama wewe na huenda na wewe ni nabiiii maaana hata humu mmejaaa tele, Mkuu wewe Kama ni mojawapo wewe endelea kuwapiga hela wasioelewa najua umejiajiri unafanya biashara ya mafuta ya arizeti wewe endelea kukanyagisha mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alaf mtu analaumu serikali kuto mshughulikia Mwamposa wakat tatizo lipo Kwa waumi wapumbavu
 
Back
Top Bottom