Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Aidha, imedaiwa kuwa washtakiwa hao walikamatwa, wakati maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakiwa katika utafiti na upelelezi kuhusianana na utoaji wa risiti za kielektroniki, waliagiza chakula na vinywaji ila walipewa risiti za mkono.
Hukumu hiyo, imetolewa Mei 08, 2026 na Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Ilala Kinyerezi, Dar es Salaam Mhe. Mohamed Burhani, baada ya washtakiwa kukiri mashtaka mawili kushindwa kutoa risiti za kielektroniki kinyume na sheria za kodi.
Hakimu Burhani alisema kesi kama hizo lazima adhabu zitolewe ili kuzuia makosa hayo yasitendwe na watu wengine.
"Kwa mujibu wa sheria sitawapa adhabu ya Magereza nitawaacha huru iwapo mtalipa faini kwa sababu mmekiri mashtaka yenu, shtaka la kwanza kila mmoja atalipa faini ya Sh milioni mbili na shtaka la pili ambalo linamkabili Fuyu peke yake atalipa Sh milioni mbili," alisema Hakimu Burhani
Hata hivyo, Hakimu Burhani aliwaeleza washtakiwa kuwa wakishindwa kulipa faini hiyo kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela, ambapo waliweza kulipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Awali, Wakili wa Serikali Salome Assey akisoma hati ya mashtaka, alidai kuwa washtakiwa hao Machi 24, 2026 katika Mtaa wa Gerezani, eneo la Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watoa huduma za chakula na vinywaji katika Kampuni ya Dicos (Mgahawa wa Kibonge), walishindwa kutoa risiti ya kielektroniki walipotoa huduma ya chakula ambayo ni sahani moja ya baga yenye thamani ya Sh.13,000.