Wauza mahindi: Hatuna mahindi tena Tanzania, yaliyopo yanatoka Zambia na Malawi

Wauza mahindi: Hatuna mahindi tena Tanzania, yaliyopo yanatoka Zambia na Malawi

Meli za mahindi ya GMO zimeanza kutua Kenya, tusishangae tutapoanza kuuziwa hayo mahindi huku kwetu.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Rift valley kenya wameanza kuvuna mahindi lakini ni machache, Nilikua naangalia wapinzani wa kule wanataka GMO isiingizwe kwao lakini tani laki mbili zimetia nanga, kenya hali ya chakula ni mbaya hasa ukizingatia wao wanakula sana ugali karibu nchi nzima ndio chakula kikuu, hata Tanzania lazima yaletwe maana ikifika january february tutaongea lugha fulani hivi nzuri kwa pamoja
 
Kwani kuna mtu amekufa kwa njaa au ameomba chakula kwa sababu ya njaa Tanzania.

kama hakuna basi nchi inajitosheleza kwa chakula
Moshi kuna kaya zinaomba chakula niliona leo hali si salama ukiwa na uhakika waache wanaopiga kelele kwa ajili ya wengine waendelee
 
Hapa ndipo Bashe alipotufikisha kwa kupenda kwake sifa.
 
Akizungumza na Azam Tv M/Kiti wa wafanyabiashara wa mazao ya chakula amedai Tanzania haina tena uwezo wa kujilisha na chakula chote hivi sasa kinatoka Nchi jirani ya Zambia na Malawi.

Ikumbukwe mapema leo akiwa kwenye ziara na Samia huko Kondoa Mkoani Dodoma Waziri mwenye dhamana ya chakula amedai nchi inajitosheleza kwa chakula.
View attachment 2424425
Serikali ya mchongo kamwe huwez ielewa. Mawaziri wankula kwa urefu wakamba zao.
Hussein Bashe ukimtafakar utajua ni mtu anajifanya hayajui maisha ya watanzania. Bashe amekuwa mtu wa kukariri kauli zake zisizokuwa na maana kwa watanzania. Jeuri, Michongo mtupu na wafanyabiashara
 
Akizungumza na Azam Tv M/Kiti wa wafanyabiashara wa mazao ya chakula amedai Tanzania haina tena uwezo wa kujilisha na chakula chote hivi sasa kinatoka Nchi jirani ya Zambia na Malawi.

Ikumbukwe mapema leo akiwa kwenye ziara na Samia huko Kondoa Mkoani Dodoma Waziri mwenye dhamana ya chakula amedai nchi inajitosheleza kwa chakula.
View attachment 2424425
Chawa huwezi waona hapa
 
Afadhali nilijua mapema na kuamua kuyajaza mahindi kwenye mifuko ya kinga njaa
Familia yangu itakula mpaka niivishe mengine
 
Wakulima ndio kwa sasa wanapelekewa mahindi ya msaada
Kuna mpumbavu mmoja chawa wa samia anasema wakulima sasa ndo mda wao wakupiga hela wanauza kwa bei wanayotaka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wako wapi waimba mapambio ya kusifia kila upuuzi 😀😀😀😁. Bado anaupiga mwingi eeeh..
 
Back
Top Bottom