DOKEZO Wauza nyama Mtwara wanatumia spray za kuua wadudu mabuchani kuzuia nzi, mamlaka ziingilie kati

DOKEZO Wauza nyama Mtwara wanatumia spray za kuua wadudu mabuchani kuzuia nzi, mamlaka ziingilie kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari wadau hili suala nimelivumilia ila nimeshindwa kulingana na masuala ya afya

Wauza mabucha wa Mtwara wakitaka kufunga bucha wanafanya usafi wa kudeki. Kisha wanachukua spray ya kuulia WADUDU kama rungu au hit wanapuliza. Kisha wanafunga.

Nasema hili sababu nimeliona kwa macho yangu

Asubuhi wakifungua harufu ya spray paint inakuwa haijaisha. Wanatundika nyama

Sasa ukienda buchani hasa mabucha ya masokoni ukivuta hewa unasikia harufu ya ile dawa na huku kuna nyama zimewekwa.

Je, ni kutokujua au makusudi hawajui kama ni simu na wanahatarisha afya za walaji

Naomba mamlaka husika zifatilie hili suala afya zetu muhimu sana kuliko pesa
 
Back
Top Bottom