TUNAKUMBUSHANA TUU
Kwa kuzingatia hayo ya hapo juu ya kuhakikisha unapata risit ya pili yenye full inf
Pia Ukienda kununua simu hakikisha
Unapewa simu kwenye boks original la simu hio
Yaani namaanisha hakikisha
Imei # iliyopo kwenye Simu ndio hio hio iliyopo kwenye boks, na tena KIUHAKIKA ZAIDI hakikisha
Imei number anayokuandikia kwenye risit yako anaisoma kutoka kwenye simu unayonunua na sio boks au iliyokosewa..
Yaani kiufupi
Kama umenunua
Simu A, hakikisha unapewa Boks A na reset A
Sasa wewe chukulia poa
Unauziwa simu kwenye Boks ambalo si la simu hio,
Na mwenzako naye kauziwa simu kwenye boks ambalo ndio lako sasa..
Siku kapoteza simu...
very simple atangalia imei kwenye boks au risit atapeleka police wata ku trace wewe...
Unakuja unatoa reset ujitetee,
Kumbe siku anaandika imei kwenye risit hukua makini ukaacha akaandika imei kutoka kwenye hilo boks lako fake(ambalo simu yake ndio imepotea sasa) na sio simu, na bahat mbaya mwenzako naye aliandikwa imei kwenye risit kutoka kwenye boks(ambalo simu yake unayo),
Kwaio boks lako(ambalo ndio la simu hio) analo yeye,
Imei ya simu hio ipo kwenye risit yake...
Yaani
Wewe unasimu A, reset B na Boks B
Mwenzako yeye ana reset A na Boks A
Hahaaaa simple logic
A goes with A's
B goes with B
Then Simple math
3 : 2
Who win???
Utatokea wapi
Boks ulilonalo linakukataa...
Risiti uliyonayo inakukataa
Simu uliyonayo inakukataa..
Maana uhalali wa simu ni unaletwa na risit na boks halali.....
Oky
Utasema basi utatumia Imei za kwenye boks/risit yako ku trace simu iliyoibiwa sasa...
Kumbuka yy anajua kbsa kaiiba....
Na anajua imei itavutwa...
Haya sasa keshaibadilisha..
Una trace unaambiwa imei haipo....
Hahhaaa aloooo aibu yote kwakooo
Sasa wewe chukulia poa uone hii ni nadharia....
Umakini huo ungekusaidia sio tuu kuepuka kuonekana mwizi bali hata wewe endapo utapoteza yako.
Za kuambiwa changanya na zako...
Neno langu si sheria..
Nimewaza tuuu..
Upendo na amani