Wauza tiketi wa usafiri wa Mwendokasi wanakera sana

Wauza tiketi wa usafiri wa Mwendokasi wanakera sana

Hayo magari ni ya kishsmba mno, hayana mfumo wa GPS, bell 🛎 hazifanyi kazi, yanajaza abiria kama ng'ombe wapelekwao machinjioni, hayana kiyoyozi, so mambo ya kuswap card hayawezi kuwemo ktk hayo magari
Nchi yetu tunaishi miaka 50 nyuma ya wakati
 
Siamini kabisa kuwa Udart wanaweza kuendesha biashara kwa kukosa chenji ya kurudisha kwa abiria wao.

Mara nyingi sana utakutana na kero la kukosekana chenji kwenye vile vibanda vya wauza tiketi vilivyoko kando ya barabara ya Morogoro hasa kwa maeneo ya Kimara Temboni, Mbezi kwa msuguri, Kibamba, Kiluvya nk.

Wakatisha tiketi wana sura ngumu, majibu ya nyodo, kebehi, dharau, huwa wanajibu kwa sauti kubwa HAKUNA CHENJI kisha wanatazama pembeni.

Hivi ni kweli wakatisha ticket Udart wanakosaga chenji? Kwa nini wakose chenji?
Wanamdharau nani wakati wao ni misukule ya kukusanya hela za watu.
 
Mtz na wizi alirogezewa kwenye wizi weka mfumo utapigwa,weka manually utapigwa, wakat mwingine waacheni wapige ili watoe huduma bora sababu Wana motisha.
 
Back
Top Bottom