Wauza uduvi jijini Dar hatarini kuolewa!

Wauza uduvi jijini Dar hatarini kuolewa!

Wauza uduvi wote Dar wapewa tahadhari ya kujiongeza vinginevyo WATAOLEWA!
hajui kuna watu wamemwomba Mungu awape hata hiyo biashara ya uduvi tu,na walivyoipata wameshukuru Mungu. duniani ukipata huwa unawaona wale wasionacho kama vile wavivu. ateme mate chini.
 
Jamaa anajisahau sana, anapata Nguvu ya kutukana watu kwa sababu ya cheo Cha Kisiasa na Cha kupewa tu!

Anafikiri watu wanapenda anavyopenda kuropoka,unawaambiaje wanaume wenzio wataolewa?!

Matusi haya na udhalilishaji!

KAZI ni KAZI tu iwe halali tu.

Kama anapitaga huku ajue amekosea sana, wauza uduvi ni watu na Wana familia zao!

Kutweza UTU wa mtu kwa sababu ya kipato chake ni kinyume hata na Imani ya Chama kilichomteua!

Lakini kwa kuwa kundi alilotukana ni wanyonge hii itapita tu.

Next time achague maneno ya kuongea kwenye kadamnasi.
 
Chalamila n lopo lopo lakin Leo kaongea kweli mtoto wa kiume lazima ufanye kaz za kiume Leo hii unakuta mtoto wa kiume anapamba ukumbi
Tuliza kisharwara hicho,Kazi za kiume ndio zipi hizo?
Watu wakijishughulisha mnasema wataolewa,Kazi za kuwaajiri hakuna!
Tambua tumetofautiana vingi kuanzia elimu mpaka ufahamu.
Heshimu KAZI yoyote halali anayofanya Binadamu,mtu hajaja kukuomba chochote unamsimangia na kumdhihaki kwa lipi?!
Not fair.
 
Hivi huyu ni maneno yake au ni AI...maana hii ni Video ya pili..

Si maneno ya Mkuu Wa Mkoa haya
Hakuna AI hapo ni yeye.
Unajua watu wanajisahau sana,Kuna watu wanajitafuta wanaishi chumba Cha Giza,Kodi 15k.
Maji wanachota kisima Cha tairi,yeye anazungumzia bill ya maji 30k!
Binadamu hata awe faqir huwezi kumdhalilisha kama hivi.
Mtu anapambana Leo anaambiwa ataolewa?
 
Yeye kalamba teuzi anaona Watu wote mafala, soko la ajira Tanzania ni gumu sana.
Hao ndio wana shauri vijana vyuoni kwenye mahafali wasiombe kazi serikalini, bali wajiajiri.

Wao wakiachwa kwenye uteuzi, utaona nyuzi humu JF wakilalamikia serikali, na kila aliyeteuliwa na ubaya wake.

Ndio maana unaona nchi yenye raia milioni 60, tunatawaliwa na watu wale wale kila siku, kila term wamo, kama sio mkuu wa,wilaya, ni mkuu wa mkoa, au mkurugenzi wa halmashauri, sijui Ras na n.k.

Nchi nzuri sana hii, mkikasirika anatumwa Mwamposa kuwapoza.
 
Hakuna AI hapo ni yeye.
Unajua watu wanajisahau sana,Kuna watu wanajitafuta wanaishi chumba Cha Giza,Kodi 15k.
Maji wanachota kisima Cha tairi,yeye anazungumzia bill ya maji 30k!
Binadamu hata awe faqir huwezi kumdhalilisha kama hivi.
Mtu anapambana Leo anaambiwa ataolewa?
Alikuwa akiongea wapi..!?nipe link
 
Yeye anavyozunguka kwenye kiti ofisini na kuvimba kwenye mV8 kwa vyeo vya uteuzi ndio anafanya KAZI ya kiume?!
KIUME PESA TU,Muhimu usitoe Salio tu.
 
Unawezaje yaani kumwambia mwanaume mwenzio ataolewa kwakua anachotumia kujitafuta umekiona haitoshi yaani sio sawa na kile chako? Tuheshimiane na tuheshimu utu wa mtu. Lengo linaweza kuwa zuri ila namna ya kumfikisha ujumbe ikaharibu
 
Uduv
 

Attachments

  • Restaurant+Blog+Images+Nov+2022-640w.jpg
    Restaurant+Blog+Images+Nov+2022-640w.jpg
    58.1 KB · Views: 5
Back
Top Bottom